Francis Godwin, Iringa
Suzana Mgonakulima |
MBUNGE
wa viti maalumu mkoa wa Iringa, Suzana
Mgonakulima (Chadema), amempongeza Rais John Magufuli kwa kuwapigania
wafanyabiashara wadogo maarufu kama Machinga kwa kutaka wasinyanyasike.
Alisema Rais
Magufuli amejipambanua kuwa mtetezi wa wanyonge na hicho ndicho kilio cha
Chadema kwa miaka mingi. Akashauri wafanyabiashara hao watengewe maeneo maalumu
kama ni lazima waondolewe mijini.
Mgonakulima alisema kuwa siku zote Machinga wamekuwa
ni watu wa kunyanyasika katika nchi
yao hali iliyopelekea Chadema wakati wa Kampeni za
uchaguzi mwaka 2010 kutumia majukwaa yake ya kampeni kueleza ni namna
gani ambavyo chama hicho kingewapigania.
Alisema uamuzi wa
Rais Magufuli kuruhusu Machinga kufanya kazi
popote bila kufukuzwa ni
mzuri na umejibu kilio cha siku nyingi cha Chadema
na wafanyabiashara hao.
Mbunge huyo alisema pamoja
na Machinga kutakiwa kufanya kazi popote, ilipendeza Serikali ikawatengea
eneo maalumu kwa ajili ya shughuli zao.
Alisema inawezakana kukawa
na muda ama siku maalumu
kwa machinga kufanyabiashara katika maeneo
yaliyotengwa ili
kuwawezesha wafanyabiashara wakubwa nao
kufanya biashara na kama itabaki hivi, upo uwezekano
wa wafanyabiashara wakubwa kujiingiza katika
biashara ya umachinga kama njia ya kukwepa kodi.
0 comments:
Post a Comment