Emeresiana Athanas
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati
na Maji (Ewura), inatarajia kutoa uamuzi wa maombi ya kupandisha gharama za
umeme yaliyotolewa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), mwishoni mwa mwezi
huu.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na
Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi kuwa Mamlaka inaendelea kuyafanyia
uchambuzi wa kina maombi hayo ili kuja na mapendekezo kabla ya Januari mosi.
"Matarajio yetu ni kwamba hadi
mwishoni mwa mwezi huu, tutakuwa tumemaliza na kutangaza, na hivyo hadi Januari
yatakuwa tayari yametolewa," alisema.
Alisema bado Mamlaka iko kwenye
uchambuzi na baada ya kukamilisha uamuzi wa maombi hayo utatolewa.
Tanesco iliwasilisha maombi ya
kupandisha gharama za umeme kwa asilimia 18, ambalo ni agizo la kubadilisha bei
ya umeme la mwaka huu lililoanza Aprili mosi.
0 comments:
Post a Comment