Hajji Kameta, Daystar
Ali Hassan Mwinyi |
RAIS mstaafu
Alhaji Ali Hassan Mwinyi amesema hajutii kusaini mkataba wa Umoja wa Mataifa wa
Haki za Watoto, kwa kuwa suala la kulea watoto wa mitaani ni la jamii nzima
hivyo wapewe haki zao za msingi.
Mwinyi
aliitoa kauli hiyo jana kwenye maadhimisho ya miaka 70 ya Shirika la Umoja wa
Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) ambapo Tanzania ni mwanachama wa Umoja wa
Mataifa wa Haki za Mtoto wa mwaka 1991 ambao ulisainiwa naye na kupata baraka
zake.
Alisema
hajutii kusaini mkataba huo kwa kuwa Tanzania imedhamiria si tu kulinda na
kuendeleza haki za mtoto lakini pia kushirikiana na wadau wanaofanya kazi kwa
ajili ya watoto.
Alisema ni
wajibu wa kila Mtanzania kusaidia kudhibiti watoto barabarani, “nimefurahi sana
suala la watoto wa barabarani linafanyiwa kazi na UNICEF, lengo likiwa ni
kuhakikisha matatizo yao yanapungua kama si kwisha kabisa.”
Alitolea
mfano kuwa mwaka 1983 akiwa Rais alipata balaa la nchi kukumbwa na Ukimwi hali
iliyosababisha wazee kupoteza maisha na watoto kubaki peke yao.
“Nilishawishi
watu wachukue watoto ili wakue wapate harufu ya mazingira ya nyumbani si
kambini na baadhi ya watu walifanya na mimi ni mmoja kati yao nilichukua wawili
nikawalea wakakua na watoto wangu, wakaolewa na sasa wako makwao,” alisema.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alilipongeza
UNICEF kwa kufanya kazi kubwa ya kuhudumia watoto Ulimwenguni hususan Tanzania.
0 comments:
Post a Comment