Abraham Ntambara
WANANCHI wametakiwa kuacha dhana potofu ya kuamini kuwa
mtu anapochangia damu inampasa kufanya hivyo kila wakati kutokana na kwamba atakuwa
ukiongezeka damu mwilini kupita kiasi mara kwa mara.
Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam
na Ofisa Uhamasishaji wa
Mpango wa Taifa wa Damu Salama
Kanda ya Mashariki, Desteria Nanyanga.
Alisema dhana
hiyo ni moja ya changamoto ambayo wamekuwa wakikabiliana nayo.
“Tumekuwa
tukikabiliana na changamoto hii. Watu wanaamini ukichangia damu leo, itakubidi
kuchangia kila wakati kwa sababu usipofanya hivyo, utapatwa na matatizo kama ya
kuumwa kichwa. Leo hii naomba niwaambie hiyo dhana ni potofu,” alisema Nanyanga.
Alifafanua kuwa wanapokuwa wakipita maeneo mbalimbali
nchini katika kuhamasisha watu kujitolea kwenye zoezi la uchangiaji wa damu,
wananchi wamekuwa wakihofia kuwa wakifanya hivyo itawabidi suala hilo liwe
endelevu, kwani kutokufanya hivyo kutawaletea tatizo la kuongezeka damu.
Nanyanga aliongeza kwamba kutokana na hali hiyo watu
huamini kwamba unapochangia damu leo itatakiwa kuchangia tena kila baada ya
mwezi mmoja au miwili kitu ambacho siyo sahihi.
Alikanusha kwamba siyo kweli kwamba ukichangia damu
itabidi iwe hali endelevu kwa maisha yako yote kwa kufanya hivyo, bali unaweza
kuchangia kwa hiari yako tu.
Alieleza kuwa kutokana na maumbile ya kibaolojia,
mwanaume anaweza kuchangia damu kila baada ya miezi mitatu, huku mwanamke
akitakiwa kuchangia damu yake kwa hiari kila baada ya miezi minne.
Alisema kuwa mtu anapaswa kuonana na daktari wa masuala
ya damu ili aweze kujua kwa nini chembe chembe zake za damu zinazalisha damu
kupita kiasi ili apatiwe matibabu.
Aidha katika kuthibitisha hilo alisema kwa upande wake
hadi sasa anatakribani mwaka mmoja na nusu tangu alipochangia damu ambapo
alibainisha kuwa hadi leo hajachangia tena na hakuna mabadiliko yoyote
anayoyaona katika mwili wake.
Kuna uhusiano gani kati ya uchangiaji damu wa mara kwa mara na matatizo ya moyo?
ReplyDelete