Leonce Zimbandu
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imevitaka vyombo
vya Dola kukamata wazazi, walezi,
mangariba na
wanaoendeleza vitendo vya ukeketaji dhidi ya watoto wa kike na wasichana katika kata ya
Kivule na maeneo mengine nchini.
Agizo hilo lilitolewa jana kutokana na taarifa ya ukeketaji hivi karibuni kwenye
kata ya Kivule, Ilala, Dar es Salaam na mikoa mengine ambayo ilikaririwa na
vyombo vya habari.
Msemaji wa Wizara hiyo, Erasto Ching’oro alisema hayo alipozungumza na
gazeti hili Dar es Salaam.
Alisema athari za ukeketaji ni majeraha kwa watoto, vifo,
vilema, maradhi, ikiwamo fistula na mengineyo.
Aliendelea
kusema kuwa watoto wa kike na wanawake wamekuwa wakifanyiwa ukatili huo bila ridhaa yao
na wakati mwingine ridhaa hupatikana kwa hila, jambo ambalo ni ukiukwaji wa
haki za binadamu.
“Wizara tunaendelea
kupambana na ukeketaji na kuongeza
juhudi ya utoaji elimu kwa jamii ili kuwachukulia hatua wanaojihusisha na mila hiyo
potofu,” alisema.
Alisema
wananchi wanapaswa kushiriki kuzuia vitendo vya ukeketaji na hasa kufichua
ukeketaji na kutoa ushahidi mahakamani ili wahusika wachukuliwe hatua.
Aidha,
Wizara ilitoa rai kwa maofisa maendeleo ya jamii na maofisa ustawi wa jamii wa
mikoa, halmashauri na kata kuzuia
ukeketaji kwa kushirikiana na mamlaka husika.
Alisema
wazazi
na walezi wanatakiwa kuacha ukeketaji kwa kuwa
ni ukatili kwa watoto wa kike na kosa la jinai, vinginevyo watafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
0 comments:
Post a Comment