Daudi Manongi-MAELEZO
BODI ya Nishati Vijijini (REB), imemteua Boniface Gissima
Nyamo-Hanga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (Rea) kuziba
nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala huo Dk. Lutengano
Mwakahesya aliyestaafu mwezi Juni 2016.
Taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa bodi hiyo Dk. Gideon
Kaunda ilieleza kuwa uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria namba 8 ya
mwaka 2005 ya Nishati Vijijini katika kikao kilichofanyika Desemba 17.
Kabla ya uteuzi huu, mhandisi Nyamo-Hanga alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Mteule huyo pia ana uzoefu wa miaka 20 katika sekta ya nishati na pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali tangu mwaka 2008 alipoajiriwa Rea.
Wasifu wake
Mteule huyo ana Shahada ya uhandisi katika fani ya Umeme
na Shahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Uhandisi.
Pia, ana Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara
(MBA) zote kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akiwa pia na Stashahada ya Juu
ya Sheria na Upatanishi na Usuluhishi ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Dar es
Salaam.
Rea inaomba sekta mbalimbali kumpatia ushirikiano mhandisi
huyo ili kumuwezesha kutekeleza majukumu
0 comments:
Post a Comment