Grace Gurisha
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu
imewaachia huru wafuasi 17 wa Chadema waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya
kula njama na kufanya kosa la jinai kwa kukusanyika isivyo halal.
Uamuzi huo ulitolewa jana na hakimu mkazi
mkuu, Victori Nongwa baada ya kupitia
ushahidi uliotolewa na mashahidi watatu wa upande wa Jamhuri na kubaini kuwa hakukuwa
na aina yoyote ya ushahidi unaoonesha siku hiyo ya tukio kulikuwepo na taflani
.
Hivyo aliwaachia huru washtakiwa hao
ambao wamo wanafunzi 10 na wafanyabiashara saba, baada ya kuwaona hawana kesi
ya kujibu dhidi ya mashtaka hayo.
Washitakiwa hao, wanadaiwa kuwa
Agosti 24,2015 walitenda kosa kwa
kukusanyika katika eneo la Morocco, Dar es Salaam bila kibali na
kusababisha hofu ya usalama kwa jamii.
Miongoni mwa washtakiwa walioochiwa huru
ni Rwegasira Alex (23) Yusuph Adamu (22) Sia Jotham (21), Mariam Michael (20)
na Michael Litanda (25), Vivian Nchimbi (25), Scolastica Masanja (29) Jackline
Michael (25) Pradius Kaiza (29) Edwina Kaiza (25), Godfrey Mhando (25) na
Dickson Congress (25).
Pia, wamo Mary Malick (30) Abdallah
Hamis (28), Fortune Francis (20) Jumanne Mvuma (28), Baraka Athumani (22),
Francis Mbwilo (22) na Said Katora (30).
Washtakiwa hao walikuwa wapo nje kwa
dhamana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini
wawili kwa kila mmoja ambao wanatambulika kisheria na kila mdhamini
aliweka bondi ya Sh 800,000.
Pia, washtakiwa hao hawakutakiwa kutoka
nje ya Dar es Salaam bila ya kuwa na ruhusa ya Mahakama.
0 comments:
Post a Comment