MANISPAA ya Ilala imegoma kuingilia kati mgogoro wa
viwanja unaofukuta baada ya halmashauri hiyo kuimilikisha Kampuni ya Green
Foundation, kabla ya wakazi wa eneo hilo kulipwa fidia, akiwamo Said Andanenga
na wenzake.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Idara ya Ardhi na Upimaji
wa Manispaa ya Ilala, Paul Mbembela alipokuwa akizungumza na gazeti hili jijini
Dar es Salaam jana.
Alisema manispaa haijasaini mkataba wa upimaji wa viwanja
na wananchi, bali iliingia mkataba na Kampuni ya Green Foun-dation baada ya
kupitia vielelezo vilivyowasilishwa ofisini kwake.
“Unajua kampuni ilifuata taratibu zote ikiwamo barua ya
serikali ya Mtaa wa Mbondole, hivyo kama manispaa ilimpatia umiliki katika eneo
hilo,” alisema.
Alisema ikiwa wananchi watakuwa na vielelezo vya Green
kukiuka mkataba wao, wanapaswa kutoa malalamiko yao man-ispaa ili
yashughulikiwe kwa mujibu wa taratibu.
Awali, mmoja wa wakazi hao, Andanenga ambaye pia ni mwanachama
wa Green Foundation alisema yeye kwa niaba ya wenzake aliandika barua mara tatu
na kuzipeleka ofisi ya manispaa, lakini hazikujibiwa.
Alisema mwaka 2007 waliamua kupima eneo hilo chini ya
kampuni hiyo na kuahidiwa kupata ofa ya viwanja hivyo, wanashangaa baadhi ya
vigogo wa manispaa kugawana viwanja katika maeneo waliyotoa.
“Manispaa haiwezi kukwepa lawama wamehusika kwa asilimia
100 wakishirikiana na Green Foundation kutudhulumu haki zetu,” alisema.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbondole, Thomas Nyanduli, alisema anaufahamu mgogoro
huo, lakini anaiomba manispaa kuingilia kati ili kunusuru mapigano.
Alisema hali ni mbaya katika eneo hilo kwani baada ya
wananchi kushindwa kupatiwa ofa zao, wameamua kuuza viwanja vya aliyemilikishwa
na manispaa.
“Manispaa inapaswa kufika eneo husika kuainisha mipaka,
haiwezekani mwenye hati ya kiwanja kumkuta mtu mwingine akijenga kwenye
kiwanja, lazima ugomvi utatokea,” alisema.
0 comments:
Post a Comment