Sharifa Marira
Magdalena Sakaya |
NAIBU Katibu Mkuu wa CUF, Bara,
Magdalena Sakaya, amesema wamekubaliana na uamuzi wa kusimamisha wagombea ubunge
na udiwani uliofanywa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.
Akizungumza na waandishi wa habari jana
Dar es Salaam, Sakaya alisema wameridhia uamuzi wa Kamati ya Mashauriano uliofikiwa
Zanzibar juzi kuhusu kuanza kwa mchakato wa uchaguzi wa jimbo la Dimani ambalo
Mbunge wake, Hafidh Ally Tahir alifariki dunia.
Sakaya alisema Katiba ya CUF kipengele cha
5 inaruhusu Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar na Bara, kusimamia vikao vya mashariano
ambapo kwa upande wa Zanzibar, alialikwa Maalim Seif, hivyo kuunga mkono uamuzi
huo wa kushiriki uchaguzi na wagombea kuanza kuchukua fomu.
‘’Vikao vipo vya aina mbili, Bara na Visiwani,
hivyo walichofanya Katibu Mkuu na
wenzake, tunakiunga mkono na tumekubali kusimamisha wagombea kwenye kata zote
na sasa tuko kwenye harakati za kuchukua fomu,’’ alisema Sakaya.
Kuhusu CUF kushirikiana na vyama vingine
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika uchaguzi huo, alisema
hadi sasa hawajapokea barua kutoka chama chochote kuomba kushirikiana, hivyo
watakwenda wenyewe bila umoja huo.
‘’Tunakwenda kushinda si kushiriki, hadi
sasa hatujapokea barua yoyote kuomba kikao cha kusimamimisha mgombea mmoja,
hivyo kila chama kinajipanga kivyake, hatuwezi kushirikiana na vyama vingine
wakati hatujakaa kuzungumza na kufikia uamuzi,‘’ alisema Sakaya.
0 comments:
Post a Comment