Abraham Ntambara
Charles Mwijage |
KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimekubaliana
na Taasisi ya Biashara ya Oxford, Uingereza kufanya utafiti wa hali ya
uwekezaji kiuchumi na fursa za kibiashara nchini na ripoti kuandikwa vitabu ili
kuitangaza Tanzania katika sekta ya uwekezaji.
Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano
hayo Dar es Salaam jana, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles
Mwijage, alisema azma ya makubaliano hayo ni kuvutia wawekezaji.
“Wataalamu hawa wa watafiti kwenye
biashara na uchumi, watazunguka nchi nzima kuangalia fursa za uwekezaji na
biashara na kuwasiliana na wawekezaji wa ndani na nje,” alisema Mwijage.
Aidha, alisema alikwishamwambia Kaimu
Mkurugenzi wa TIC kuwa haridhishwi na jinsi nchi inavyojitangaza na kubainisha
kwamba kuna umuhimu wa kujitangaza.
Mwijage aliwataka watafiti hao kuleta taarifa
nzuri zitakazovutia wawekezaji huku akiwashukuru kwa kuja kufanya shughuli zao
nchini ikiwa moja ya nchi 12 ambazo tasisi hiyo inafanya shughuli zake.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TIC, Cliford Tandali alisema
makubaliano hayo ni ya miezi minane na wataanza kazi kwa kuhoji viongozi wa Serikali
wakiwamo mawaziri na wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Shirika la Maendekleo ya
Petroli Tanzania (TPDC).
0 comments:
Post a Comment