Abraham Ntambara
Boniphace Jacob |
MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya
Ubungo, Boniphace Jacob, amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
hana mamlaka ya kumuagiza kuhakikisha anamaliza changamoto ya madarasa matano
katika Shule ya Sekondari Urafiki.
Kauli hiyo aliitoa jana wakati
akizungumza na JAMBO LEO ambapo alisema mkuu huyo wa mkoa alipotoa agizo hilo
hivi karibuni wakati wa ziara yake alikuwa akijifurahisha.
"Kwanza hana mamlaka ya kuniagiza,
alikuwa anajifurahisha tu, alikuwa anafurahisha baraza hana mamlaka hayo ya
kuniagiza," alisema Jacob.
Aidha alilisisitiza kwa kusema kuwa mkuu
wa mkoa hana mamlaka ya kuwaambia jambo lolote lile hivyo hawezi kutii agizo
lolote ambalo limetolewa na mtu asiye na mamlaka dhidi yake.
Meya Jacob alimshauri Makonda kufanya
shughuli zinazomhusu tu,kwa kuwa kila mtu anamajukumu yake yaliyoainishwa
kisheria ambapo alibainisha kuwa hakuna sheria iliyotoa maelekezo kuwa atakuwa
na mamlaka ya kumuagiza meya.
Aliongeza kama halmashauri wanamipango
yao na kwamba wanatumia fedha zao ambapo alibainisha kuwa yeye kama mwenyekiti
wa mipango hiyo na kusema kuwa yeye ndiyo mwenyekiti wa vikao vya halmashauri
na kwamba hakuna mahal palipoainishwa wao kulazimika kutekeleza mipango ya
serikali.
Alifafanua kuwa hata ujenzi wa shule
hiyo ulifanywa kwa nguvu zao wenyewe kama wananchi na kusema kwamba fedha za
halmashauri kwa ajili ya maendeleo wanazikusanya wenyewe na kupanga namna ya
kuzitumia hivyo kama mkuu wa mkoa hatakiwi kuziingilia wa kuzifuatilia namna
zinavyotumika.
Meye huyo wa Ubungo alisema hadi sasa
wanaushirikiano mzuri na Mkuu wa Wilaya hiyo Hamphrey Polepole na kwamba hakuna
baya lolote ambalo kashamfanyia tofauti na wakati yupo Kinondoni ambapo hakuwa
na ushirikano mzuri na viongozi wa serikal.
Itakumbukwa kwamba hivi karibuni wakati
wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alipotembelea wilaya ya Ubungo
alimuagiza Meya wa Halimashauri hiyo ambaye pia ni diwani wa kata ya Ubungo
Boniphace Jacob kuhakikisha anamaliza changamoto ya madarasa matano katika
shule ya Sekondari Urafiki.
"Diwani wa hapa anatakribani miaka
mitano hivyo inabidi apambane na kuhakikisha uhaba wa vyumba hivyo vitano
unakamilika"
0 comments:
Post a Comment