Abraham Ntambara
Dk Hamisi Kigwangala |
SERIKALI
imepiga marufuku uuzaji wa vilainishi vya kupima unaofanyika mtaani na sokoni
kwa sababu vifungashio vya vilainishi hivyo havikidhi ubora na vinaharibu
vilainishi ambavyo huathiri utendaji wa mitambo.
Aidha, imemwagiza
Mkemia Mkuu wa Serikali kuendelea na uchunguzi wa kimaabara wa vilainishi
vilivyo sokoni, kwa kushirikiana na kampuni zenye nembo halisi ili kubaini na
kutambua bidhaa za vilainishi halisi na visivyokidhi viwango vya ubora.
Kauli
hiyo ilitolewa juzi Dar es Salaam kwa vyombo vya habari na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Dk Hamisi
Kigwangala, wakati akitoa tamko kuhusu ubora wa bidhaa za vilainishi nchini kwa
mwaka 2013 hadi mwaka huu.
“Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Maabara ya Mkemia
Mkuu wa Serikali inatekeleza jukumu la kusimamia Sheria Namba 3 ya mwaka 2003
inayohusu Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani.
“Lengo
kuu la kuanzishwa kwa sheria hiyo ni kuhakikisha nchi inalindwa ili isiwe soko
la bidhaa hafifu, kemikali zinazoingia
na kutumika nchini ziwe zenye ubora na salama katika kulinda afya na mazingira,”
alisema Dk Kigwangala.
Alisema Maabara
ya Mkemia Mkuu wa Serikali ilipofanya ufutiliaji wa ubora wa vilainishi
vinavyouzwa sokoni na kuvifanyia uchunguzi ili kubaini kama vimekidhi viwango vya
ubora katika Jiji la Dar es Salaam, na kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara,
ilibaini asilimia 50 ya vilainishi vya injini na petroli zilizochunguzwa
ilionekana kutokidhi viwango vya ubora.
Aidha
aliongeza kwamba asilimia 52.6 ya vilainishi vya injini, aina ya dizeli
vilivyochunguzwa vilionekana kutokidhi viwango vya ubora vya vilainishi vya
kitaifa huku asilimia 77.7
ya vilainishi aina ya ATF vilionekana kutokidhi viwango vya ubora.
0 comments:
Post a Comment