Mariam Cyprian, Tanga
JUMLA ya kesi 20,601 zimeripotiwa mkoani
hapa katika kipindi cha Januari hadi
Novemba, ikiwa ni pungufu kwa kesi 565 ikilinganishwa na kesi 2016
zilizoripotiwa mwaka 2015.
Takwimu hizo zilitolewa na Kamanda wa
Polisi mkoani Tanga, Benedict Wakulyamba wakati akitoa taarifa ya hali ya
usalama kwa waandishi wa habari ofisini kwake.
Wakulyamba alisema kuwa kati ya kesi
hizo 20,601 zilizofunguliwa, Jumla ya kesi 7,056 zilifikishwa mahakamani na
kesi 2,198 washtakiwa wake walitiwa hatiani na kupewa adhabu mbalimbali.
Alisema wastakiwa wa kesi 1,472 waliachiwa
huru na Mahakama kwa sababu za kisheria. “Kesi nyengine ziko katika hatua
mbalimbali za uendeshaji.
Aidha Kamanda huyo alisema kuwa katika
kipindi hicho Jeshi la Polisi liliendesha misako na operasheni mbalimbali na
kufanikiwa kukamata wahalifu waliofanya au kutaka kufanya vitendo vya uhalifu
ikiwa ni pamoja na vielelezo mbalimbali vya kesi zao.
Akizungumzia kwa upande wa wahamiaji
katika kipindi hicho alisema walikamata wahamiaji haramu 168; kati yao
wahamiaji 73 Wasomalia, kumi Waethiopia na wengine Wakenya.
Aidha kwa upande wa madawa ya kulevya, kamanda
huyo alisema kesi za bangi 294 zilifunguliwa kwenye vituo vya Polisi ambapo
Bangi yenye uzito wa kg 1,188.2 ilikamatwa na kulikuwa na kesi 165 za mirungi
“Lakini pia kwa upande wa madawa ya kulevya ya
viwandani jumla ya kesi 54 zilifunguliwa, zikihusisha kukamatwa kwa jumla ya gramu
130.48 za madawa ya kulevya,” alisema RPC huyo.
Hata hivyo, Kamanda huyo alisema pia
katika kipindi hicho walifanikiwa kukamata silaha za moto 37 katika kupambana
na uzibiti wa matukio ya ujambazi na unyang’aji kwa kutumia silaha ikiwa ni
mkakati wa kukabiliana na vitendo vya uhalifu mkoani hapa ili kuhakikisha vinamalizika.
Sambamba na hilo lakini pia Jeshi hilo
lilifanikiwa kukamata risasi ambapo kati ya hizo risasi 425 zilikuwa za
SMG,Risasi 24 zilikuwa za Shotgun na
Risasi 25 zilikuwa ni za Rifle.
Alisema kuwa katika kipindi hicho silaha
ambazo zimekamatwa ni SMG nane,Marker IV
mbili,Shotgun nne,Pistol moja na Rifle
mbili ambazo zilikamatwa kwenye matukio
mbalimbali yaliyokuwa yakitokea mkoani hapa.
Aidha alisema katika ya silaha hizo pia
mabomu manne ya kurusha kwa mkono na
Gobore ishirini zilikamatwa kwa watuhumiwa wa uhalifu mkoani hapa ambayo
yalikuwa yakitumika kufanyia vitendo vya uhalifu.
"Katika kipindi hicho tuliweza
kukamata risasi 425 za SMG, risasi 24 za shotgun na risasi 25 za rifle
zilizokamatwa kutokana na misako mbalimbali iliyofanywa na Jeshi la Polisi
kwenye matukio mbalimbali,” alisema RPC Wakulyamba.
0 comments:
Post a Comment