Mwandishi Wetu
Dk. John Magufuli |
OFISI ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora imetangaza uteuzi wa makatibu tawala wa wilaya 27 kujaza
nafasi zilizokuwa zimeachwa wazi.
Makatibu tawala hao na wilaya zao katika
mabano ni Timotheo Mzava (Arumeru, Arusha), Fabian Sospeter (Nyangw’hale, Geita
), Innocent Nsena (Karagwe), Abdallah Mayomb (Misenyi), Greyson Mwengu (Kyerwa),
Agnes Mwakyoza (Biharamulo), Mbwana Kambangwa (Liwale), Agenellus Mwakitalu
(Kilwa), Sarah Sanga (Hanang’), Paul Bura (Mbulu), Yohana Kastila (Kilosa).
Wengine ni Robert Selasela (Kilombero),
Lameck Lusesa (Malinyi), Palango Abdul (Nanyumbu), Bosco Bugali (Misungwi),
Menruf Nyoni (Magu), Said Kitinga (Ilemela), Grace Mgeni (Makete), Zaina Mlawa
(Ludewa), Milongo Sanga (Kibiti), Frank Sichalwe (Kalambo), Nicodemas Mwikozi
(Meatu), Filbert Kanyilizu (Itilima).
Pia wamo Godwin Chacha (Busega),
Winfrida Funto (Ikungi), Elizabeth Rwesagira (Mkalama), Michael Nyahenga
(Kaliua).
Taarifa iliyotolewa jana na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela
Kairuki inawataka makatibu tawala hao kufika kwa Katibu Mkuu wa Wizara wakiwa
na wasifu wao (CV) na nakala za vyeti vyao vya kielimu.
0 comments:
Post a Comment