Richard Mwangulube
Mbunge huyo amelazimika kukwama kutoka rumande kwa kipindi kirefu kutokana na lugha zake tata kwa viongozi wa Serikali wa wilaya na mkoa.
Mara kadhaa Lema ameshindwa kupata dhamana mahakamani kwa takribani zaidi ya mwezi tangu alipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza.
Jambo lingine ambalo lilitikisa mkoa huo na taifa kwa ujumla ni utata wa Faru John kama ilivyoanishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea mamlaka ya hifadhi ya Ngorogoro. Faru John amezua utata mkubwa serikalini na wizara husika ya Maliasili na Utalii.
Jambo jingine ambalo limeutikisa mkoa na taifa pamoja na tasnia ya habari nchini kote ni la kuwekwa rumande mwandishi wa habari wa redio one na ITV, Khalfan Liundi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti.
Liundi anadaiwa kuwa alikwenda katika
vijiji vya wilaya ya Arumeru na kuandika habari za uchochezi. hatua hiyo
imedaiwa na mkuu huyo wa wilaya kuwa ni kuingilia uhuru wa habari.
Mkoa wa Arusha katika mwaka huu wa 2016 pia umetikiswa na kuzuka kwa ugonjwa hatari wa Kimeta (ANTHRAX) ambao umeua wanyamapori wengi katika Wilaya ya Monduli.
Ugonjwa huu mbali na kuua wanyamapori na mifugo pia uliathiri sekta ya utalii katika kipindi kifupi tangu uzuke.
Sekta ya utalii ilitikiswa zaidi katika hifadhi ya Manyara katika Vijiji vya Selela hali ambayo ilipunguza idadi ya watalii waliotembelea baadhi ya vivutio katika hifadhi ya Manyara.
Katika kukabiliana na ugonjwa huu Wataalam kutoka taasisi mbalimbali zinazohusiana na sekta ya wanyamapori na mifugo kulazimika kutumwa katika wailaya ya Monduli ili kudhibiti ugonjwa huo
0 comments:
Post a Comment