Mery Kitosio, Arusha
MTUHUMIWA wa uchochezi, Mbunge wa Arusha
Mjini, Godbless Lema, ataaga mwaka huu na kukaribisha mpya akiwa gerezani.
Hali hiyo ilijidhihirisha jana baada ya
kurudishwa gerezani Kisongo, kutokana na Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya
Arusha, kusikilioza hoja za opande mbili kwnye kesi yake na kuamua kutioa
uamuzi Januari 4.
Awali Mahakama hiyo ilisikiliza maombi
ya notisi ya rufaa yaliyowasilishwa na upande wa Jamhuri na wa mshitakiwa
Lema na pande hizo kukubaliana kusikilizwa rufaa ya upande wa Jamhuri huku wa
Lema ukiiomba Mahakama kuwasilisha wake kesho kwa maandishi.
Hata hivyo, baada ya kukamilika kwa hoja
hizo za kujibizana kwa maandishi ndani ya siku mbili uamuzi wa rufaa hiyo sasa
ikaonekana utatolea Januari 4.
Rufaa hizo ni pamoja na ya Jamhuri
kutoridhika na uamuzi wa Jaji Dk Modesta Opiyo wa kuwapa siku 10 akina Lema kuwasilisha
notisi ya rufaa na upande wa mshitakiwa ni ile ya kupinga uamuzi wa Mahakama ya
chini kushindwa kumpa Lema masharti ya dhamana.
Jaji aliyesikiliza rufaa hizo, Salma
Magimbi alisema baada ya upande wa Jamhuri kuwasilisha rufaa kwa njia ya
maandishi upande wa Lema utaijibu Desemba
30 huku Januari 2 pande hizo zikikutana kufanya majumuisho na uamuzi wa rufaa
hizo kutolewa Januari 4.
Baada ya kusikiliza rufaa hizo, Mahakama
iliibua hoja yenyewe na kuwapa kazi mawakili wa pande hizo kuangalia na kutoa
hoja kuhusu uhalali kisheria kuhusu notisi iliyotolewa na Serikali kama ilikuwa
na mashiko ya kisheria.
Wakili wa mshitakiwa, Peter Kibatala
alisema upande wake uliiomba Mahakama kusubirisha rufaa yao ili wasikilize
rufaa ya upande wa Jamhuri kwani rufaa zote ziligongana na kuelekea sehemu moja.
"Unajua leo rufaa mbili zimegongana;
ya Jamhuri na yetu, hivyo tumeiomba Mahakama isitishe yetu ili isikilizwe
ya Jamhuri kwanza, kwani rufaa zote zinaelekea upande mmoja,wa ndege apande
ndege na wa basi apande basi, la msingi tunaelekea sehemu moja sote,"
alisema Kibatala.
Lema alirudishwa tena kwenye gereza la
Kisongo hadi Januari 4 Mahakama hiyo itakapotoa uamuzi wa rufaa hiyo.
0 comments:
Post a Comment