Celina Mathew
Zitto Kabwe |
MBUNGE wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo),
Zitto Kabwe ametaka Watanzania wajiwekee utaratibu wa kusoma vitabu huku
akibainisha kuwa mwaka huu alisoma vitabu 53, idadi aliyodai kuwa hakupata kuifikisha
huko nyuma.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya
habari, Zitto alisema aliamua kusoma idadi hiyo ya vitabu mwaka huu ili mwakani
apate wakati mzuri wa malezi baada ya mkewe kujifungua.
"Mwaka huu nimeongeza idadi ya
vitabu nilivyosoma tofauti na mwaka jana, lakini sikufikia idadi ya mwaka juzi
ambapo nilisoma 56. Hiyo ndiyo rekodi ya juu zaidi tangu nilipoanza kuorodhesha
vitabu nilivyosoma mwaka 2012. Mwaka 2013 niliorodhesha vitabu vichache
zaidi," alisema.
Alisema mwaka huu ulimfunua kuhusu uwezo
mkubwa na umahiri wa wachapishaji wa vitabu wa ndani na kwamba alipata fursa
adhimu ya kuzungumza na Walter Bgoya wa kampuni ya uchapishaji ya Mkuki na
Nyota.
Alisema alijifunza mengi mapya ya
historia ya nchi na Afrika na kwamba kisa kilichomchekesha ni anapokumbuka
hadithi ya Rais Seretse Khama wa Botswana alivyobeba machungwa kwenye ndege
kumletea zawadi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere akimtania kuwa sera zake za
Ujamaa zilileta njaa nchini.
0 comments:
Post a Comment