Ibrahim Yassin
WAKAZI wa kijiji cha Kateka kilichoko
katika Kata ya Matai wilayani Kalambo wameingia kwenye wakati mgumu baada ya makazi
yao kuharibiwa na mvua kubwa iliyokuwa imeambatana na upepo mkali.
Mvua hiyo imeezua mapaa ya nyumba 17 na
kufanya wakazi wake wakose makazi katika kipindi hiki cha mvua za masika.
Wakizungumza na gazeti hili huku wakilia,
baada ya kutokea kwa adha hiyo walisema mvua hiyo iliyonyesha ghafla, imefanya uharibifu
mkubwa katika eneo hilo.
Juma Mwanalinze alisema kuwa mvua hiyo ilinyesha
kwa muda wa dakika thelathini tu lakini imefanya uhalibifu mkubwa.
Wakazi hao wameiomba Serikali kuwasaidia
kupata mahala pa kujihifadhi katika kipindi hicho cha mvua, kwani hawana na
namna ya kufanya kwa ajili ya kujisiri.
Afisa tarafa ya Matai, Andrew Manyema Ngindo,
licha ya alisema baada ya kutokea adha hiyo walitoa taarifa kwa mkuu wa wilaya hiyo,
Julieth Binyura samba samba na kutoa taarifa kwenye uongozi wa halmashauri husika.
Alisema viongozi wote walifika eneo la tukio
na kushuhudia zaidi ya kaya kwenye eneo hilo zikiwa zimehalibiwa vibaya na kusema
mpaka sasa kamati ya maafa imekaa ili kutathmini watu walioathirika na janga hilo
na kuangalia namna ya kuwasaaidia.
Alisema chanzo ni kutokana ni wananchi
wengi kujenga nyumba zisizo kuwa imara.
Mkuu wa wilaya hiyo, Julieth Binyula
alisema ameanza ziara ya kuangalia maeneo yote yaliyokubwa na kadhia hiyo na kuahidi
kutoa taarifa zaidi, baada ya kumaliza uchunguzi na kufanya tathmini kwa wathirika
wote.
Alisema ipo haja ya wananchi kupanda
miti kwa wingi ili kuzuia upepo unaoharibu makazi na kuwa makazi mengi
yameharibiwa kutokana na maeneo mengi kutokuwa na miti.
0 comments:
Post a Comment