Salha Mohamed
Ramadhani Kailima |
KAMPENI za uchaguzi mdogo katika Jimbo
la Dimani kwa ngazi za ubunge na udiwani zinaanza rasmi leo.
Jimbo hilo lenye kata 20 linatarajia
kufanya uchaguzi wake Januari 21, huku kata mbili za Mkoma na Mwamtani
zikitolewa kwenye uchaguzi huo.
Akizungumza jana Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uhaguzi (NEC), Ramadhani Kailima, alisema kampeni
hizo za kuchagua mbunge na madiwani zitakamilika Januari 21.
Alisema licha ya kuanza kwa kampeni leo
orodha ya majina ya wagombea itawekwa wazi leo asubuhi.
“Kampeni za uchaguzi zitaanza kesho (leo)
uteuzi wa wagombea mwisho ni leo (jana)
saa 10 jioni na orodha itatolewa kesho (leo) asubuhi,” alisema Kailima.
Katika uchaguzi huo, kata za halmashauri
za Tanzania Bara ni 20 zitashiriki, huku NEC ikibainisha kuwa kanuni ya 18(2)
ya Uchaguzi wa Rais na Wabunge ya Mwaka 2015 inaalika asasi na taasisi za ndani
zitakazokuwa watazamaji wa uchaguzi huo.
0 comments:
Post a Comment