Mwandishi Wetu
Balozi John Kijazi |
RAIS John Magufuli amemteua Jaji wa
Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) na wengine sita katika nyadhifa tofauti na wanatarajiwa
kuapishwa leo.
Jaji Kaijage anachukua nafasi ya Jaji
mstaafu Damian Lubuva ambaye muda wake wa kuwa Mwenyekiti ulimalizika rasmi
Desemba 19.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, kupitia Mkurugenzi wa Mawasiliano ya
Rais, Ikulu Gerson Msigwa ilieleza kuwa Jaji Kaijage aliteuliwa kuongoza Tume
hiyo kwa miaka mitano kuanzia Desemba 20.
Aidha, Rais Magufuli alimteua Jaji mstaafu
Hamid Hamid kuwa Makamu Mwenyekiti wa NEC kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Jaji mstaafu Hamid alikuwa Makamu
Mwenyekiti wa NEC na kumaliza kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano Desemba
19.
Hali kadhalika, alimteua Jaji mstaafu wa
Mahakama ya Rufaa, Harold Nsekela kuwa Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa miaka mitano kuanzia Desemba 20.
Jaji mstaafu Nsekela anachukua nafasi
iliyoachwa wazi na Jaji mstaafu Salome Kaganda aliyestaafu Desemba 10.
Katika hatua nyingine, Rais aliteua majaji
wanne wa Mahakama Kuu kuwa majaji wa Mahakama ya Rufaa ambao uteuzi wao ulianza
jana na ni majaji Dk Gerald Ndika, Jackobs Mwambegele, Rehema Mkuye na
Sivangilwa Mwangesi. Wateule hao wanatarajiwa kuapishwa leo Ikulu, Dar es
Salaam.
0 comments:
Post a Comment