Grace Gurisha
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imeshindwa
kutoa uamuzi wa kama itafuta mashitaka ya mauaji dhidi ya mke wa marehemu
bilionea Erasto Msuya, Miriam Msuya (41) anayetuhumiwa kumuua dada wa marehemu,
Aneth.
Hiyo inatokana na Mahakama hiyo jana kukwama kutoa
uamuzi, ikiwa ni mara kadhaa sasa tangu Agosti 10 ilipotakiwa ifanye hivyo kwa
mara ya kwanza.
Hakimu Mkazi, Magreth Bankika amekuwa akiiahirisha kesi
hiyo mara kadhaa na baadaye kuihamishia Mahakama nyingine ambako ilipangiwa
Godfrey Mwambapa, lakini bado uamuzi haujatolewa kila ikija inaelezwa kuwa bado
uamuzi haujakamilika.
Kesi hiyo ilikuja jana mbele ya Hakimu Mwambapa, ambapo
aliahirisha hadi Desemba 29 atakapotoa uamuzi.
Hatua hiyo ilifikiwa na Mahakama hiyo, baada ya Wakili wa
Miriam, Peter Kibatala kuwasilisha ombi hilo mbele ya Hakimu Mkazi Magreth
Bankika kuwa hati ya mashitaka ina kasoro na kuomba ifutwe pia akidai kuwa
wateja wake waliteswa na polisi.
Mbali na Miriam, mshitakiwa mwingine ni mfanyabiashara wa
Arusha, Revocatus Muyela (40), ambapo Kibatala alidai pia kuwa washitakiwa hao
waliteswa na askari kabla ya kuchuliwa maelezo, ili wakiri kuhusika na mauaji
hayo.
Akijibu hoja hizo, Wakili wa Serikali, Diana Lukondo alifdai
hati ya mashitaka iliyo mahakamani hapo iko sahihi kwa kuwa ina sababu zote za
kuitwa hati ya mashitaka, kwa hiyo hoja za Kibatala hazina mashiko.
Muyela aliunganishwa katika kesi hiyo, baada ya kukamatwa
na kubainika kuwa anatuhumiwa na mauaji hayo. Aneth ni dada wa marehemu
bilionea Msuya, na alichinjwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake Kibada,
Block 16, Kigamboni, Dar es Salaam Mei 26.
0 comments:
Post a Comment