Emeresiana Athanas
TAASISI ya Sekta Binafsi Tanzania
(TPSF), imesema inatarajia kuanza utekelezaji wa utoaji wa elimu ya
ujasiriamali kwa watumishi wa umma ili waweze kuanzisha biashara watakapo
staafu.
Aidha inatarajia pia kutoa elimu ya
ujasiriamali kwa vijana, mradi ambao utasaidia kutokomeza suala la ukosefu wa
ajira kwa vijana kwa kuimarisha utendaji
uliosheheni uadilifu.
Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa
hafla ya kumtambua mjasiriamali mahiri wa mashindano ya Ujasiriamali Barani
Afrika Jenifer Shigholi, Mwenyekiti wa Bodi ya TPSF, Salum Shamte alisema kuwa
watumishi wa umma wakiandaliwa vizuri watachangia maendeleo ya taifa kutokana
na upeo wako kuwa mkubwa.
"Elimu hii itawapa uwezo kwa
kutumia mbinu mbalimbali kwa kuanzisha biashara watakazoweza kusimamia,
kuziendesha na kuwaletea maisha bora," alisema.
Kuhusu vijana alisema kuwa elimu hiyo
itampa mbinu bora ya matumizi ya fedha na rasilimali mbalimbali ili aweze
kujiajiri wenyewe na kutengeneza ajira kwa wenzao.
"TPSF kwa kushirikiana na Wizara ya
Kazi, Ajira, Sera na Walemavu iko mbioni kukamilisha programu ya mafunzo ya
kazi ya awali inayolenga vijana wahitimu ili waweze kupata ujuzi wakati
wanasubiri kupata ajira," alisema.
0 comments:
Post a Comment