Peter Akaro
George Masaju |
OFISI
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imesema haina mamlaka ya kuzuia wala kuruhusu
mtumishi yeyote wa Serikali kukopa au kutokukopa katika taasisi yoyote ya
kifedha nchini.
Imetoa
kauli hiyo baada ya siku za karibuni kuenea taarifa iliyodaiwa kutoka ofisi
hiyo kuwa Serikali imepiga marufuku watumishi wa umma kukopa benki, Saccos, vicoba
na taasisi mbalimbali za kifedha.
Kwa
mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari ilitolewa jana Dar es Salaam na Naibu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Asiatu Msuya, taarifa hiyo siyo ya kweli.
“Ikumbukwe
kuwa mikopo yote ya watumishi wa umma katika taasisi za fedha hutolewa kwa
kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo ili mradi mtumishi awe ametimiza
vigezo,” alisema.
Msuya
aliongeza kuwa watumishi wa umma wasijihusihe na usambazaji wa taarifa zisizo
za kweli na ambazo hazijatolewa na mamlaka husika.
0 comments:
Post a Comment