Abraham Ntambara
Zitto Kabwe |
CHAMA cha ACT Wazalendo kimeendelea
kulaani ukoloni wa Morocco kwa taifa la Sahara Magharabi na kimepinga juhudi
zozote zinazofanywa na Serikali za kufifisha msimamo wa nchi kwa visingizio vya
diplomasia ya uchumi.
Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari
jana Dar es Salaam na Katibu wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Chama hicho John
Mbozu ilisisitiza juu ya msimamo wa Tanzania kuhusu Uhuru wa Sahara Magharibi.
"Tunalaani ukoloni wa Morocco kwa
taifa la Sahara Magharibi, tunapinga juhudi zozote za kufifisha msimamo wetu kwa
visingizio vya diplomasia ya uchumi, ACT Wazalendo tuko Pamoja na Watu wa
Sahara Magharibi dhidi ya ukoloni wa Morocco," alisema Mbuzi.
Mbozu alieleza msisitizo wa mafungamano
kati ya Tanzania na Watu wa Sahara Magharibi.
Alisema uongozi wa ACT Wazalendo mapema
mwakani, unatarajia kufanya ziara maalumu ya kutembelea maeneo yaliyokombolewa
na kushikiliwa na Chama cha Polisario ili kujionea maendeleo ya harakati za ukombozi
na kuziunga mkono.
Mbuzu alieleza kuwa viongozi wa chama
ambao wanahudhuria Mkutano Mkuu wa Vyama vya Kijamaa unaoendelea jijini Berlin
Ujerumani, walifanya mazungumzo ya kina na viongozi wa Chama cha Kijamaa cha
Polisario kinachopigania Uhuru wa nchi ya Sahara Magharibi inayokaliwa kimabavu
na Morocco.
Alikumbusha kwamba Sera ya mambo ya nje
ya nchi yetu Tanzania tangu wakati wa Baba wa Taifa ni kusimama na wanyonge na
kubainisha kuwa msingi huo bado ni muhimu.
Alisema kwa sababu hiyo, ACT-Wazalendo
walipinga ujio wa Mfalme wa Morocco nchini kwa kuwa taifa hilo bado linaikalia
ardhi ya watu wanyonge wa Sahara Magharibi.
0 comments:
Post a Comment