Moses Ng’wat, Kyela
Freeman Mbowe |
MWENYEKITI wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amevunja uongozi wa
chama hicho wilaya ya Kyela na kuteua safu mpya ili kunusuru chama hicho
kupasuka kutokana na makundi yaliyotokana na uchaguzi mkuu uliopita.
Katika safu hiyo
mpya itakayongozwa na mwanasiasa mkongwe, Lumuli Kasyupa, ambaye amewahi kuwa
mbunge wa Kimbo la Kyela na Naibu Waziri wa Kilimo katika Serikali ya Awamu ya Kwanza
ya hayati Mwalimu Julius Nyerere, kabla ya kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM)
na kujiunga na Chadema.
Uamuzi huo wa
Mbowe ulifanyika juzi kwenye ziara yake na mikutano ya ndani inayoendelea
mkoani Mbeya kwa lengo la kukijenga chama hicho na kushughulika na mambo
mbalimbali.
Mbali na Kasyupa
ambaye alikuwa kada wa CCM na mbunge wa jimbo la Kyela kwa miaka 15, wengine
waliochaguliwa ni Makamu Mwenyekiti, Philimon Mahenge, Katibu ni Mponjoli
Mwaikimba, wakati katibu wa uenezi ni Donald Mwaisango maarufu kama Alfa na
Omega na mweka hazina, Timoth Luvanda.
Wenyeviti wa
mabaraza walioteuliwa ni mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (Bawacha), Tamali
Mwambalaswa, Bavicha ni Yesaya Mwakalobo na Mwenyekiti wa Baraza la wazee Anton
Mapunda.
Hata hivyo,
Mbowe alionekana kukasirishwa na migogoro iliyokithiri ndani ya chama hicho na
kusababisha kishindwe kufikia malengo yake ya kushika dola,
huku akitumia nafasi hiyo kuwaonya madiwani kwa uzembe.
0 comments:
Post a Comment