Grace Gurisha
KESI ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) na Mhariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina
inatarajia kuanza kusikilizwa Januari 18, 2017 baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Jabir Idrisa na
Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.
Upande wa Jamhuri ulidai jana mbele ya Hakimu Mkazi
Mwandamizi Thomas Simba kuwa kesi ilikuja kwa kusikilizwa, lakini hawana
mashahidi kwa hiyo wanaomba wapangiwe tarehe nyingine ya kuendelea kusikiliza
kesi hiyo.
Hakimu alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo
hadi mwakani, ambapo washitakiwa hao waliwakilishwa na Peter Kibatala. Awali,
hakimu huyo alishangaa upande wa Jamhuri kushindwa kumkamata Lissu licha ya
kwamba yeye alitoa hati ya kukamatwa kwa Mbunge huyo.
Hata hivyo, alimueleza Lissu kuwa aachane na mambo
anayofanya kwa sababu yeye ni kioo cha jamii, kwa hiyo hastahili kufanya
anayoyafanya na pia yeye ni mwanasheria na ajua sheria.
Ilidaiwa Januari 12 hadi 14, 2016 katika jiji la Dar es
Salaam, washtakiwa watatu, Jabir, Mkina na Lissu, kwa pamoja waliandika na
kuchapisha taarifa? za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko
yaja Zanzibar’.
0 comments:
Post a Comment