Peter Akaro
Maxence Melo |
KAMANDA
wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, amesema hawezi
kuzungumzia tuhuma za kukamatwa kwa Mkurugenzi wa Mtandao wa Jamii Forums,
Maxence Melo, huku akiwatoa hofu waandishi juu ya kauli ya Mzee wa Upako.
Akizungumza
jana Dar es Salaam wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari, Sirro alisema
tuhuma la kukamatwa na kushikiliwa kwa Melo atazitolea ufafanuzi Ijumaa.
Alipoulizwa
na waandishi juu ya kauli ya Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo
Kibangu, Anthony Lusekelo kuwa waandishi waliomwandika vibaya watakufa, Sirro
alisema kauli hiyo inaweza kumpa hofu mpagani tu.
“Kwa
hiyo mpagani akisikia kauli ya mtu mwingine mpagani kwa sababu anafikiria
upagani wake, ataanza kuwa na wasiwasi.
“Lakini
kwa sababu unajua Mungu ni huyu mmoja, na yeye ndiye amekuleta duniani na yeye
ndiye atakutoa duniani, hupaswi kuwa na hofu,” alisema Sirro.
Katika
hatua nyingine, watu 22 wametiwa nguvuni na Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam, kwa tuhuma za wizi kwenye taa za kuongozea magari.
Kamanda
Sirro alisema watuhumiwa hao wamekuwa wakipora wananchi wenye magari na wapita
njia kwenye taa hizo.
“Wamekuwa
wakijiunga vikundi na kupora mali ndani ya magari zikiwamo simu za mkononi,
kompyuta mpakato, saa na fedha,” alisema.
Alisema
Desemba 11, Keko Magurumbasi na taa za Veta Chang’ombe, Temeke walikamata
watuhumiwa 10.
Alitaja
baadhi ya wahutumiwa hao kuwa ni Ayubu Amiri (19), Shabani Fadhili (18) na
Herman Francis (26).
“Katika
mahojiano, walikiri kujihusisha na makosa mbalimbali yakiwamo ya unyang’anyi wa
kutumia silaha na nguvu.
“Uchunguzi
wa awali ulibaini kuwa Francis anakabiliwa na tuhuma za mauaji, ambapo Machi 20
alimchoma mtu kisu na kutoroka,” alisema Sirro.
Aliongeza
kuwa msako uliofanyika Desemba 12 Veta ya Chang’ombe ulikamata watuhumiwa
wengine 12 kwa wizi kutoka kwenye magari.
Baadhi
yao ni Sande Kassim (18), Emmanuel Abel (21), Paulo Abel (18), Jafari Nyerere
(22), Hamisi Salum (22) na Hemedi Idrisa (22).
0 comments:
Post a Comment