MAMIA
ya wakazi wa Kijiji cha Mbigili na mji wa
Ilula katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, wamefurika
katika mazishi ya aina yake yaliyofanyika katika
kitongoji cha Mkawaganga Kijiji cha Mbigili Wilaya
ya Kilolo mkoani Iringa kushuhudia mazishi ya kihistoria ya
mzee mmoja aliyefariki dunia ghafla na kuzikwa kaburi moja na kondoo na
kuku mweusi.
Tukio
hilo limetokea jana wakati wa mazishi ya mzee huyo, Andrea
Ngaga (90) mkazi wa kitongoji cha Mkawaganga aliyekuwa
akijishughulisha na kazi za uganga wa kienyeji kijijini hapo
enzi za uhai wake .
Baadhi ya
wananchi waliofika katika mazishi hayo walisema
kuwa walilazimika kusitisha shughuli zao za
shamba na biashara na kufika kushuhudia mazishi hayo ambayo
ni mara ya kwanza kufanyika katika kijiji hicho.
Mmoja wa
mashuhuda wa tukio hilo, John Mfaligoha alisema kuwa kabla
ya kifo chake marehemu aliwaeleza namna mazishi yake
alivyotaka yawe.
Kwa sababu
kulikuwa na taarifa hizo, wananchi wakatamani kufika ili waone aina hiyo ya
mazishi, alisema.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Kijiji cha Mbigili, Ibrahim Rashid
(46) alisema amezaliwa katika kijiji hicho miaka mingi,
lakini tukio hilo ni la kwanza kuliona na kusikia.
Hata hivyo
alieleza kuwa mazishi hayo yamefanyika kimila zaidi na mara nyingi
mahala pengine marehemu anachagua mtu wa kuzikwa naye kabla
ya kifo .
“Huyu (marehemu)
hakuweka maagizo, alisema tua angetamani kuzikwa kimila na hizo ndizo mila za
eneo hili,” alisema mwenyekiti huyo wa kijiji na kubainsha kuwa
aliyeongoza mazishi hayo ni mganga wa kienyeji kutoka
Ifunda wilaya ya Iringa aliyemtaja kwa jina la Galasiano
Mfaume Nyeza ambaye ni baba mdogo na marehemu huyo.
Mtendaji
wa Serikali ya kijiji hicho, Thabith Kalolo alisema
kimsingi hakuna kosa lolote, kwani serikali haiingilii uhuru
wa wananchi wake kuamini masuala ya mila na kuwa
iwapo mazishi hayo yangekiuka haki za binadamu mwingine;
mfano kama wangemzika na binadamu mwingine aliyehai, hapa
isingewezekana ila kwa kumzika na kondoo na kuku mweusi
hakuna shida .
Hata
hivyo, alisema tofauti ya rekodi ya misiba iliyopata
kutokea katika kijiji hicho, msiba huo umevunja rekodi
kwa kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watu.
“Tumezoea
rambirambi za misiba kuwa ni kati ya Sh300,000 na Sh500,000, lakini msiba huo
rambirambi zimefika Sh1.3 milioni. Hii ni dalili kwamba msiba huu umekusanya
watu wengi sana,” alisema.
Mtoto wa
marehemu, Kurugenzi Ngaga alisema kuwa baba yake
alifariki dunia juzi saa 6 usiku baada ya kusumbuliwa na chembe ya moyo. Alisema marehemu ameacha
wajane wawili na watoto 19.
Kurugenzi
alisema kimila kama ingekuwa zamani, marehemu
angezikwa na mjukuu wake aliyemteua kushika mikoba yake, ila
kutokana na mambo ya mila kwa sasa kupewa kisogo, waliona ni
vema wakamzika na kondoo na kuku huyu mweusi.
0 comments:
Post a Comment