Mwandishi Wetu, Zanzibar
Maalim Seif |
MAJINA ya wagombea ubunge katika Jimbo
la Dimani kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) yametangazwa.
Mgombea wa CUF ni Abdulrazak Khatib
Ramadhan na wa CCM ni Juma Ali Juma na wote wamesema wako tayari kwa kampeni zinazoanza
kesho.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor
Ahmed Mazrui, aliiambia JAMBOLEO juzi kuwa Baraza Kuu la CUF lilimteua Ramadhan
kuwania ubunge wa Dimani.
“Jumapili mgombea tuliyempitisha alichukua
fomu ya uteuzi kwenye ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Wilaya ya
Magharibi B,” alisema Mazrui.
Mgombea wa CCM naye alichukua fomu kwenye
ofisi za muda za NEC katika sekondari ya Kiembe Samaki na sasa wanasubiri uchaguzi
pekee.
Mbali na uchaguzi mdogo wa ubunge Dimani
pia NEC itaendesha uchaguzi wa udiwani kwenye kata 22 nchini ambapo jumla ya
Sh. bilioni tatu zitatumika.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhan
Kailima alisema maandalizi ya uchaguzi huo yamekamilika, ambapo Sh bilioni 1.7
zitatumika kwenye uchaguzi mdogo wa Dimani na Sh bilioni 2.2 zitatumika kwa uchaguzi
wa udiwani kwenye kata 22.
Fomu zilianza kutolewa Desemba 15 ambapo
mwisho itakuwa ni Desemba 22 na kampeni zitaanza rasmi Desemba 23 hadi Januari
21.
Uchaguzi mdogo wa Dimani unafanyika
kutokana na kifo cha Hafidh Ali Twahir aliyefariki dunia Novemba 11 kwenye hospitali ya rufaa ya
Dodoma.
0 comments:
Post a Comment