Mwandishi Wetu
Zitto Kabwe |
KIONGOZI wa ACT-WAzalendo, Zitto Kabwe, ameishauri
Seikali kuandaa kanuni za kuhakikisha kila hospitali ina akiba ya kutosha ya
damu ili kusaidia wagonjwa wenye kuhitaji kabla watu wengine hawajajitolea ili
kuokoa maisha.
Zitto ametoa ushauri huo jana kupitia waraka wake kwa
njia ya mtandao ambapo pia aliihimiza jamii kuongeza bidii ya kuchangia dau kwa
hiyari kufuatia tukio aliloshuhudia katika moja ya hospitali Dar es Salaam,
usiku wa kuamkia jana ambapo wazazi wawili walikuwa wakihaha kusaka msaada wa
damu kuokoa maisha ya mtoto wao.
“Naishauri Serikali itengeneze kanuni za kuhakikisha kila
hospitali inakuwa na akiba ya damu ya kutosha na mgonjwa mwenye kuhitaji apewe
kwanza damu kabla ya kutafuta watu wa kuchangia kiwango husika.
Juhudi za kuchangia damu kwa hiari ziongezeke kama
tufanyavyo wanachama wa ACT Wazalendo ambao kila mwaka wiki ya kwanza ya
Mwezi Mei hujitolea damu kwa hiari kwenye hospitali za umma nchini kote,”
alisema.
Zitto pia amewashauri Watanzania kujua makundi ya damu
waliyonayo na kuweka kumbukumbu ili waweze kuokoa maisha yaw engine au yao
pindi damu itakapotakiwa kwa haraka.
“Sasa najua Group langu, ilikuwa ni makosa makubwa na
uzembe wa hali ya juu kwangu kutojua ' blood group ' yangu. Msiojua ‘blood
group’, mjue sasa kwani hatujui siku wala saa,” alisema Zitto baada ya kupima
na kujitolea damu kuokoa maisha ya mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la
Rahma.
0 comments:
Post a Comment