Abraham Ntambara
WAGONJWA
wa Kisukari nchini wameendelea kuhimizwa kujiunga na mifuko ya Bima ya Afya ili
kukabiliana na changamoto ya gharama za matibabu.
Mratibu
wa Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza kutoka Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mariam Kalomo alimwambia
mwandishi wa habari hii ingawa kwa sasa watoto na watu wa umri chini ya miaka
26 wanapatiwa matibabu bure, wagonjwa wengi bado wanalazimika kulipia huduma
hiyo.
“Kama ni
mtoto basi yeye anauhakika wa kupata matibabu bure kwenye ile mikoa ambayo ina
kliniki kwa sababu zinasaidiwa na shirika la kisukari duniani. Lakini wajiunnge
kwenye mifuko ya bima ya afya, sasa hivi wametoa fungu la watoto, ipo ya Sh.
50,000,” Kalomo.
Dk.
Kalomo alisema kuwa vipimo kwa wagonjwa wote wa kisukari wamekuwa wakipatiwa
bure, isipokuwa dawa hususani kwa watu wazima ndiyo wamekuwa wakilazimika
kujinunulia wanyewe.
Aidha
alikumbusha kwamba Sera ya Serikali ni kuhakikisha wagonjwa wa magonjwa sugu
ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa kisukari inatakiwa matibabu yao yawe bure, lakini
inabaki kuwa changamoto na kutokidhi mahitaji, hivyo kuwataka watu wazima
kujihudumia wenyewe katika matibabu.
Dk.
Kalomo aliongeza kuwa Serikali imejipanga vizuri ili kusaidia katika matibabu
ya magonjwa sugu kama hayo ndiyo maana Serikali imeongeza fungu katika bajeti
ya mwaka 2016/2017 ambayo itasaidia katika ununuzi wa dawa.
Alisema Shirika
la Kisukari Duniani (World Diabetes Federation) ndiyo ambalo limekuwa likisaidia
kuchangia batibabu ya bure kwa wagonjswa wa kisukari nchini hususani kwa watoto
na watu wa chini ya umri wa miaka 26.
Alibainisha
kwamba nzima nzima ina kliniki takribani 40 tu zanazotoa huduma ya ugonjwa wa
kisukari ambapo alisema zinapatikana kote Tanzania Bara na Visiwani hususani
katika hospitali za mikoa na wilaya.
Dk.
Kalomo alisema kliniki hizo zimekuwa zikipata misaada kutoka katika Shirika
hilo ya dawa, Sirinji pamoja na vifaa vya vipimo vya ugonjwa huo kutoka katika ambavyo
vyote, wagonjwa hususani wa watoto na watu wa chini ya umri wa miaka 26
huhudumiwa bure.
Aidha
alisema pamoja na shirika hilo kutoa mchango wake nchini bado kuna wakati kuna
kuwa na changamoto ya kukosekana kwa dawa hali ambayo hupelekea wagonjwa
wanaofaidika matibabu ya bure kulazimika kujinunulia dawa.
0 comments:
Post a Comment