Peter Akaro
Paul Makonda |
MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amekabidhi vitu vyenye thamani ya zaidi
ya Sh milioni 164 alivyoahidi kwenye ziara zake na pikipiki tano kwa Saidi
Mrisho aliyetobolewa macho na ‘Scorpion’.
Kuanzia
Novemba 19 hadi 28, Makonda alifanya ziara katika wilaya za Dar es Salaam kujua
matatizo ya wananchi na kuahidi kutekeleza baadhi ya mambo.
Akizungumza
jana, Makonda alisema ameona ni vema akaanza kutekeleza baadhi ya ahadi zake kabla
mwaka kumalizika, huku mambo mengine yakisubiri utekelezaji kutoka ngazi za juu
za uongozi.
Makonda
alikikabidhi kituo cha kurekebisha tabia cha Kigamboni magodoro 50, runinga,
king’amuzi, mitungi miwili ya gesi na jiko.
Pia
alikabidhi gari la kubeba wagonjwa kwa Jeshi la Polisi Kikosi cha Kutuliza
Ghasia (FFU) Ukonga, na tumba za kwaya ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Sekondari
ya Jitegemee ilipewa mabati 2,000, shule ya msingi Mbagala Annex mabati 1,000,
shule ya Katoliki mifuko 10,000 ya saruji, soko la samaki Msasani mabati 300,
kanisa la AIC matofali 10,000 na mabati 200 kwa ajili ya Uwanja wa Taifa.
Katika
kuthamini viongozi wanaojituma, alitoa pikipiki kwa mtendaji wa kata ya Mbuyuni
na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Buguruni.
Pia
hakuwaacha nyuma wajasiriamali kwani alimkadidhi Lumino Evance mtaji wa Sh
milioni moja na mama muuza machungwa Zuhura Waziri mtaji wa Sh 200,000.
Kutokana
na changamoto ya maji Ukonga, Makonda alikabidhi Sh milioni 13 ili wananchi wa
Gongo la Mboto na Pugu wapate maji. Pia alitoa Sh 500,000 kwa ajili ya
kukamilisha tangi la maji kwa wananchi wa Buyuni, kata ya Pemba Mnazi.
Aidha,
Makonda alitoa zawadi kwa watumishi wanne waliokuwa tayari kujitolea na kufanya kazi kwa ufanisi,
ambao walizadiwa kulala siku moja kwenye
hoteli ya kifahari kwa gharama ya zaidi ya Sh milioni tano.
Kuhusu
Mrisho ambaye alishindwa kuhudhuria hafla hiyo na kuwakilishwa, Makonda alisema
utaratibu wa kumtafutia nyumba kama alivyoomba unaendelea.
Aliongeza
kuwa kilichokwamisha ni eneo alilochagua ambalo walikuta lina mgogoro, hivyo alisema
wanamtafutia sehemu nyingine kwa sasa.
Baada
ya makabidhiano hayo baadhi ya wanufaika walimshukuru Makonda kuwa mwenye moyo wa
uthubutu.
Kamanada
wa FFU Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Stanley Kukaganeo alisema gari
walilokabidhiwa litasaidia kuokoa maisha ya wananchi wengi wanaohitaji msaada
wa dharura.
“Tumekuwa
tukiumia sana mgonjwa kufia mikononi mwetu kwa sababu ya kukosa gari la kumwahisha
hospitali ila Mkuu wa Mkoa tulikueleza hilo na sasa umetekeleza, ahsante sana,”
alisema.
Zuhura
alisema hakuwahi kufikiria kitu kama hicho katika maisha yake na anaona ni
bahati kupata msaada huo.
“Niliomba
Sh 20,000 ila wewe (Makonda) umenipa Sh 200,000, Mungu akubariki na uendelee na
moyo huo huo wa kutusaidia,” alisema.
0 comments:
Post a Comment