Hussein Ndubikile
Mohamed Mpinga |
KAMANDA wa Kikosi cha Usalama Barabarani,
Mohamed Mpinga, amesema kwa muda wa miezi sita jeshi hilo limekusanya Sh bilioni
28.5 zilizotokana na tozo za faini za makosa ya barabarani.
Makusanyo hayo yalianzia mwezi Januari
hadi Juni mwaka huu kwa kutumia mfumo wa mashine za kielektroniki.
Akizungumza na JAMBO lEO jana alisema makusanyo ya fedha hizo kwa kiasi
kikubwa yamechangiwa na makosa yaliyofanywa na waendesha daladala, pikipiki na
bajaj zinazofanya shughuli katika jiji la Dar es Salaam na magari ya watu
binafsi.
"Kuanzia Januari hadi Juni kikosi
cha usalama barabarani kimekusanya fedha hiyo yote na hiyo imewezekana kutokana
na umakini wa askari wetu,” alisema.
Kamanda Mpinga alisema jeshi hilo
halitawafumbia macho madereva wa vyombo vyote vya moto watakaokiuka sheria za
barabarani kwa kuwafikisha mahakamani.
Wakati huo huo, amewataka watumiaji wa
vyombo vya moto katika kipindi cha Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya kuwa
makaini kwani kikosi hicho kimejipanga
kuhakikisha hakuna ajali za kizembe zinazoweza kutokea.
Pia, hivi sasa idadi ya askari wa
barabarani imeongezwa na ukaguzi wa leseni za udereva unaendelea ili kuwabaini
madereva wasio na vigezo na kuwachukulia hatua za kisheria.
Aliongeza kuwa madereva wa mabasi
watakaobainika kuendesha zaidi ya mwendokasi wa kilomita 90 kwa saa kinyume na
makubaliano yaliyofikiwa kati jeshi hilo na wamiliki wa mabasi watakamatwa na
kufikishwa mahakamani.
0 comments:
Post a Comment