Venance Nestory
Balozi Augustine Mahiga |
TANZANIA
na Kenya wametia saini ya uundwaji wa Tume ya pamoja itakayoleta maboresho
katika mazingira ya uwekezaji, biashara na kuongeza fursa za ajira kwa vijana
baina ya nchi hizo mbili.
Utiaji saini huo ulifanywa mwishoni mwa wiki
kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Tanzania,
Balozi Augustine Mahiga na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa
wa Kenya, Balozi Amina Mohamed.
Awali,
marais wa nchi hizo Uhuru Kenyata (Kenya) na Rais John Magufuli, walikutana na
kukubaliana kuendeleza kukuza uhusiano wao ambao ulianzishwa tangu enzi wa waasisi
wa nchi hizo mbili.
Katika
mkutano wa tatu wa Tume ya pamoja ya Ushirikiano, walikubaliana katika sekta ya
Nyumba na Maendeleo ya vijiji, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT),
Uvuvi, Mazingira, Usafiri wa mjini na Sekta ya Nishati na Madini.
Pia,
mkutano huo uliamua kuweka mfumo wa ufuatliaji wa karibu wa makubaliano hayo
yaliyofikiwa chini ya Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje ya nchi hizo. Chombo
hicho kitakuwa kikikutana kila baada ya miezi sita.
Wachambuzi
wameeleza kuwa makubaliano hayo yataleta msukumo mpya baina ya nchi hizo mbili
katika kuimarisha urafiki wake na kukuza dhana ya ujirani mwema.
Tanzania
na Kenya ikakubaliana kuendeleza ushirikiano wao katika Jumuiya ya Afrika
Mashariki, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa katika kujikwamua kiuchumi na
maendelea ya nchi hizo mbili.
0 comments:
Post a Comment