Grace Gurisha
Maxence Melo |
HATIMAYE
muasisi wa mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo, ameachwa huru kwa dhamana na
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, baada ya kukaa mahabusu kwa siku sita akishikiliwa na
Polisi kwa mahojiano.
Melo
aliachwa jana na Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa, baada ya kutimiza masharti ya
dhamana ya wadhamini wawili wa kuaminika ambao walisaini bondi ya Sh milioni
tano kila mmoja, huku pia akitakiwa asitoke nje ya Dar es Salaam bila kibali
cha Mahakama.
Baada ya
mshitakiwa huyo kupata dhamana, ndugu, jamaa na marafiki walishindwa kujizuia
wakaangua vilio vya furaha huku wakipongezena kwa kufanikisha dhamana ya ndugu
yao.
Wakati
Melo akitoka eneo hilo alionekana dhahiri kupepesuka, hali ambayo ilisababisha
watu waliomzunguka wakiwamo baadhi ya wanasheria wake kumshikilia huku wengine
wakimpa pole.
Melo
akiwa mbele ya Hakimu Mwambapa, alidaiwa kuwa katika tarehe zisizofahamika kati
Mei 10 na Desemba 13 alizuia upelelezi wa Jeshi hilo akikataa kukubaliana na
amri za kutoa taarifa alizonazo kwenye mtandao wake.
Alidai
kuwa akiwa ofisini kwake Mikocheni, akifahamu kuwa Polisi inachunguza makosa ya
mitandaoni kupitia tovuti yake kinyume na sheria ya makosa mitandaoni, alikataa
kutoa taarifa hizo za elektroniki.
Mbali na
mashitaka hayo, pia anadaiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Thomas Simba, kwa
mujibu wa Wakili wa Serikali Mwandamizi Mohamed Salum kuwa tarehe
zisizofahamika kati ya Aprili mosi, na Desemba 13,Mikocheni, akiwa Mkurugenzi
wa Jamii Media Ltd ambaye ni mwendeshaji
mtandao wa kijamii wa Jamii Forums alizuia upelelezi.
Katika kesi
ya tatu, Melo alipandishwa kizimbani kujibu tuhuma mbele ya Hakimu Victoria
Nongwa ambapo akituhumiwa mara mbili; kwanza kuzuia upelelezi na pili kuendesha
mtandao bila kuusajili.
Salum
alidai kuwa katika tarehe zisizofahamika, kati ya Desemba 9, 2011 na Desemba 13
mwaka huu akiwa Mikocheni aliendesha mtandao wa ‘jamiiforums.com’ bila
kusajiliwa katika mtandao wa Tanzania (do-tz). Melo alikana mashitaka.
0 comments:
Post a Comment