Mchele wa plastiki |
WATANZANIA wametakiwa kutoa taarifa
wanabaini uwepo wa mchele usioeleweka, baada ya kuibuka kwa taarifa ya mchele
bandia wa plastiki kukamatwa Nigeria.
Msemaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa
(TFDA), Gaudencia Simwanza alisema hayo jana alipozungumza na mwandishi wa
gazeti hili.
Alisema wao sasa wana mifumo mizuri ya
kudhibiti uingizwaji wa bidhaa zisizofaa na mpaka sasa mfumo huo haujabaini
mchele wa aina hiyo nchini.
"Tunadhibiti na tuko makini
kufuatilia wafanyabiashara wanaoingiza vitu haramu na kama huo mchele ungekuwa
umeingia, tungeshajua," alisema.
Mwandishi wa habari hii alipomwuliza
ikitokea umeingizwa kimagendo nchini, Watamzania watautambua vipi, Gaudencia
aliwataka kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa watakapoona mchele wasiouelewa.
Mchele huo bandia ulikamatwa na Mamlaka
ya Mji wa Lagos, Nigeria wiki hii, ambapo walikamata magunia 102.
Taarifa kutoka nchini humo, zilieleza
kuwa uliingizwa nchini humo na wafanyabiashara haramu na unafanana na mchele wa
kawaida, hivyo ni ngumu kuutofautisha na mchele wa kawaida.
Kutokana na kusambaa kwa kasi kwa mchele
huo, huwezi kuutambua kwa haraka hadi pale unapopikwa ndipo unaweza kuona ni
mchele wa plastiki. Hata hivyo baadhi ya wataalamu walisema kabla ya kuupika
mchele huo ukilowekwa kwenye chombo chenye maji unaelea tofauti na halisi ambao
huzama.
0 comments:
Post a Comment