Grace Gurisha
Josephat Gwajima |
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat
Gwajima, ana kesi ya kujibu katika kesi inayomkabili ya kutohifadhi bastola sehemu
salama.
Hiyo ilibainika jana baada ya Mahakama kupitia mashahidi
watano wa upande wa Jamhuri.
Uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian
Mkeha wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, ambapo alisema Gwajima
na wenzake watatu watatakiwa kujibu mashitaka yanayowakabili baada ya kupitia
ushahidi.
Wakili wa washitakiwa hao, Peter Kibatala alidai kuwa watakuwa
na mashahidi watatu wakijumuishwa na washitakiwa, watakuwa saba, ambapo wote
wanne watajitetea chini ya kiapo.
Awali, Mpelelezi wa Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam, Sajini Albogast alidai kuwa wasaidizi wa Askofu
Gwajima walimpelekea bastola saa nane usiku hospitalini TMJ alikokuwa amelazwa
baada ya kuanguka akiwa kituo cha Polisi akihojiwa.
Shahidi huyo alitaja wasaidizi hao kuwa ni Yekonia
Bihagaze, George Mzava na Geofrey Milulu, ambao walitenda kosa hilo kinyume cha
sheria kwa sababu kwa hali ya kawaida, haiwezekani mgonjwa kupelekewa silaha.
Alidai kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kinondoni alimuunganisha
na Mkuu wa Kituo cha Kawe, Pamphil ambaye alimkabidhi begi lililokuwa na silaha
bastola namba CAT 5802, risasi tatu zilizokuwa kwenye magazini, CD mbili, risasi
17 za bastola na kitabu cha umiliki wa silaha, nguo ya ndani na hati ya
kusafiria ya Mchungaji huyo.
0 comments:
Post a Comment