Apandishwa kortini akidaiwa kulawiti


Mary Mtuka

MKAZI wa Kinondoni 'B' Jijini Dar es Salaam Sajala Binde (34), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni akituhumiwa kumwingilia kinyume na maumbile mwanamke mmoja (jina limehifadhiwa).

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Is -Haq Kuppa, Wakili wa Serikali, Joseph Nasuwa alidai kuwa tukio hilo lilitokea Juni 6 mwaka huu maeneo ya Kinondoni Biafra.

Baada ya kusomewa hati hiyo ya mashitaka, mtuhumiwa alikana kutenda kosa hilo na Wakili alidai upelelezi bado unaendelea.

Hakimu Kuppa alisema shtaka hilo linadhaminika kisheria, hivyo alimtaka mtuhumiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua ya utambulisho na kujidhamini kwa Sh. milioni tano kila mmoja.

Hata hivyo, mshitakiwa huyo alishindwa masharti ya dhamana na kurudishwa rumande ambapo Hakimu Kuppa alihairisha kesi hiyo hadi Desemba 20, mwaka huu.

Wakati huohuo, Husaein Yusuph (17) na rafiki yake Emmanuel Cosmas wamepanaishwa kizimbani katika mahakama hiyo wakikabiliwa na kupatikana na madawa ya kulevya yenye uzito wa Gramu 32.1.

Wakisomewa maelezo ya kosa mbele ya Hakimu Boniface Lihamwike, Wakili wa Serikali Ramadhan Mkimbu, alidai kwamba watuhumiwa walitenda kosa hilo Novemba 13 mwaka.

Wakili Mkimbu alidai kuwa watuhumiwa walipatikana na madawa hayo aina ya Cannabis Sativa yajulikanayo kwa jina la Bhangi.

Baada ya kusomewa shtaka hilo kila mmoja kwa wakati wake alikana kutenda kosa hilo na Wakili alidai upelelezi bado unaendelea.

Hakimu Lihamwike alisema kesi hiyo inadhaminika kisheria hivyo aliwataka watuhumiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua watakao weka saini ya Sh. milioni 1 kwa kila mmoja.

Hata hivyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 12 mwaka huu na watuhumiwa walirejeshwa mahabusu.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo