Francis Godwin, Iringa
Dk. John Magufuli |
BARAZA
Kuu la Umoja wa Wanawake Mkoa wa Iringa limetoa
tamko kumpongeza Rais John Magufuli kwa kutimiza mwaka mmoja madarakani.
Aidha,
limempongeza pia Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa mkoa huo,
Jesca Msambatavangu kwa kuwa kiongozi wa mfano ndani na nje
ya Iringa, huku wakimwomba kugombea tena nafasi hiyo katika
uchaguzi mwakani 2017 .
Mwenyekiti
wa UWT wilaya ya Mufindi Marcelina Mkini ambaye pia ni
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
CCM Taifa (Nec), alisema kuwa ushindi ambao CCM iliupata
katika uchaguzi mkuu mwaka jana ulitokana pamoja na mambo mengine, kazi
nzuri iliyofanywa na Msambatavangu.
Alisema
mkoa wa Iringa kwenye uchaguzi huo ulifanya vizuri kwa
kushinda majimbo sita kati ya saba na kuwa pamoja na
kila mmoja kushiriki katika kupigania ushindi huo wa
chama, wanawake hawanabudi kumpongeza mwanamke mwenzao ambaye ndiye
mwenyekiti wa chama mkoa
''Naomba
kuchukua nafasi hii kwa niaba ya wanawake wenzangu
kukupongeza sana mwenyekiti wetu wa CCM mkoa Jesca Msambatavangu. Umeonyesha
mfano mzuri kuwa unaweza kuongoza .......nakumbuka wakati wa
kampeni wewe ulisimama kidete kuhakikisha
chama kinashinda kwa kishindo mbali ya figisu figisu
zilizokuwa zikielekezwa kwao ila hukuteteleka ''
Mbali na
mwenyekiti huyo kufanya vema katika kampeni za 2015,
bado aliendelea kuitumikia jamii ya mkoa wa Iringa. “Mwenyekiti
wetu anafanya kazi vizuri ndani ya mkoa
wetu tena pasipo ubaguzi wowote na ni mtetezi
mzuri sana kwa wanawake ndani ya mkoa na hanaga unafiki
kabisa kwani yeye siku zote husema
kweli tupu ''
Mkini
alisema kuwa kutokana na utendaji kazi wake
mzuri ndani ya chama wao wanaona bado
mwenyekiti huyo ana uwezo wa kuwavusha wana CCM kwa miaka
mingine mitano ijayo, hivyo kumshawishi kuingia tena
ulingoni mwakani 2017 katika uchaguzi mkuu wa viongozi
ngazi mbali mbali za chama .
Mwenyekiti
wa UWT mkoa wa Iringa Zainab Mwamwindi akisoma tamko la
UWT mkoa wa Iringa kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt
Magufuli alisema kuwa wao kama wanawake wa
CCM wameendelea kufurahishwa na utendaji kazi wa Rais Dkt
Magufuli na kuwa kubwa zaidi ni jinsi Rais
alivyoweza kujibu maswali ya watanzania kupitia
mkutano wake wahariri wa vyombo mbali mbali
vya habari hapa nchini.
Msambatavangu
alisema atahakikisha pongezi za wanawake hao zinamfikia Rais Dkt Magufuli
huku akiwasisitiza wanawake kuendelea kuongoza
nafasi zao kwa kujiamini.
Alisema
wakati chama kinajiandaa kwa chaguzi zake mwakani ni vizuri
wanawake kuanza kujipima ama kuwapima wale ambao
wanaingia kuwania nafasi mbalimbali ili kupata viongozi wenye
uwezo wa kuwatumikia wananchi.
0 comments:
Post a Comment