Hussein Ndubikile
Profesa Sospeter Muhongo |
WASOMI nchini wamesifu utendaji kazi
wa mwaka mmoja wa Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuwa amejaribu kuendana na kasi ya Serikali
katika usambazaji umeme vijijini, upatikanaji wa umeme na kupunguza gharama.
Akizungumza na JAMBO LEO jana, Mhadhiri
wa Sayansi ya Siasa na Utawala Bora wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard
Mbunda alisema katika kipindi hicho, Waziri Muhongo ameonesha wazi kujali
wananchi.
Alisema Waziri amefanya kazi kubwa ya
kusaidia kupunguza makato ya umeme yaliyokuwa yakiumiza wananchi na kasi ya
usambazaji umeme kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA).
"Ameonesha wazi ni kiongozi
anayejali wananchi wake kwa kuwapunguzia ukali wa makato ya umeme na hata
usambazaji umeme vijijini kasi yake inaridhisha," alisema.
Alisisitiza kuwa Waziri Muhongo amefanya
kazi ya kujali maslahi ya wananchi kwa kuzuia upandishaji bei ya umeme nchini
na amefanikiwa kuondoa utata uliokuwapo katika kashfa ya Akaunti ya Tegeta
Escrow.
Aliyekuwa Mjumbe wa Bunge la Mabadiliko
ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu alisema Waziri huyo ameboresha vyanzo vya uzalishaji
nishati hiyo ikiwamo mitambo ya kuzalisha umeme ya Kinyerezi I na II Dar es
Salaam hali ambayo imeimarisha upatikanaji umeme.
Alimshauri Profesa Muhongo kuendelea
kukuza vyanzo hivyo, ili tatizo la kukatika umeme liwe historia.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Hamad
Salim alisema ni miongoni wa viongozi wanaoendana na kasi ya Rais John Magufuli
katika utekelezaji wa ahadi likiwamo suala la uunganishiaji umeme kwa wananchi
wa vijijini.
0 comments:
Post a Comment