Mwandishi Wetu, Nairobi
Ummy Mwalim |
MAWAZIRI wa afya wa nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC), wamepitishe sera ya afya na mwongozo na mkakati wa afya
ya mama, mtoto na vijana.
Sera na mwongozo huo vimepitishwa katika
kikao cha mawaziri hao kilichofanyika nchini Kenya ambapo Waziri wa Afya Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu aliongoza kikao hicho.
Waziri Mwalimu alisema kupitia sera na
muongozo huo makundi husika yatapata unafuu wa huduma za afya kwa kuwa
zitasimamia utekelezaji wa mpango wa kuboresha na kuimarisha afya katika nchi
wanachama.
“Sera hizi zitasimamia utekelezaji wa
mipango ya kuboresha na kuimarisha afya katika nchi wanachama wa jumuiya kwa utaratibu
unaofanana,” alisema.
Alisema mkutano huo wa mawaziri pia ulichambua
na kupitia taarifa ya makatibu wakuu wa wizara zao ambapo ulieleza kuridhishwa
na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa maagizo ya mawaziri wa afya ikiwemo
kuanzishwa kwa mpango wa pamoja wa kusimamia dawa, mpango wa pamoja wa kukagua vyuo
vikuu vya afya pamoja na mpango wa pamoja wa huduma za ukimwi/VVU.
“Taarifa ya ukaguzi wa vyuo vikuu vya afya
vya Tanzania itawasilishwa katika kikao cha 14 cha mawaziri wa afya wa EAC
kitakachofanyika Burund Machi, mwakani,” alisema.
Mwenyekiti huyo wa mkutano aliwataka
mawaziri wenzake kutekeleza maamuzi waliyokubaliana katika mkutano huo ili
kutimiza kwa vitendo matarajio ya wananchi wa EAC kuwa na afya bora.
“Mkutano huo ulitanguliwa na kikao cha
wataalam na kikao cha makatibu wakuu wa wizara za afya katika nchi wanachama
vilifanyika kuanzia Novemba 14 hadi 17, mwaka huu,” alisema.
Mkutano huo ulihudhuriwa na mawaziri wa
afya wa Kenya, Burundi, Uganda pamoja na Mwakilishi wa Waziri wa Afya wa
Rwanda.
0 comments:
Post a Comment