Mary Mtuka
Edda Sanga |
MTANDAO wa wadau katika asasi za kiraia
umeiomba Serikali kuboresha miundombinu
ya barabara zinazojengwa kuzingatia matumizi ya watumiaji wote na kuzifanya
salama kwa wote.
Kauli hiyo imetolewa wakati wa
maadhimisho wa siku ya kuwakumbuka wahanga wa ajali za barabarani, ambayo
hufanyika Novemba 20 kila mwaka.
Akizungumza Dar es Salaam jana katika
maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Chama Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania
(Tamwa), Edda Sanga alisema Serikali inawajibika kuzifanya barabarani kuwa
sehemu salama kwa kila mmoja.
Alisema ajali za barabarani zimekuwa na
athari nyingi hapa nchini kiuchumi na kijamii, kwani takwimu zinaonesha kuwa
takribani watu milioni 1.24 duniani hufariki kila mwaka kutokana na ajali.
"Mtandao wa wadau kutoka asasi za
kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusiyo usalama barabarani
Tanzania, kama ilivyo ratibiwa na Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania
(Tawla) tunaomba serikali na watunga sheria kuifanyia maboresho ya sheria ya
usalama barabarani ya mwaka 1973," alisema.
Mkurugenzi huyo alisema maeneo ya
maboresho ya sheria hiyo ni pamoja na mwendokasi ambao umekuwa sababu kubwa ya ajali zinazogharimu uhai wa watu
wengi.
Mkurugenzi wa Programu kutoka Tawla
Nasieku Kisambu alisema katika kuadhimisha siku hiyo wanaomba kuwepo kwa
usimamizi wa usalama wa vyombo vya moto vinavyo ingia nchini, ili kujua kama
vitamlinda mtumiaji pindi inapotokea ajali.
Pia alisema Serikali inapaswa kuwa na
magari ya kutoa hudumia ya kwanza baada ya ajali kutokea kwani ni moja ya
changamoto nchini.
Kwa upande wake mmoja wa wahanga wa
ajali Salumu Haji alitumia fursa hiyo kushukuru msaada alioupata kutoka Tamwa tangu alipo pata ajali mwaka 2012.
"Nilipata ajali na nikapoteza mguu
wangu mmoja na kusababisha kukimbiwa na mke wangu na kuniacha na watoto wa
wawili wanao nitegemea hadi "
alisema.
Hata hivyo alisema anaiomba serikali na
watu wengine kumsaidia kuweza kujiajiri ili kuweza kuwahudumia watoto wake,
hata ikiwezakana kupata bajaji.
0 comments:
Post a Comment