Mery Kitosio, Arusha
Mawakili wa Serikali Paulo Kadushi na Materus Marando jana waliwasilisha hoja ya kupinga pingamizi hilo mbele ya Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Sekela Moshi kwamba maombi ya upande wa Lema kufanya mapitio si sahihi kwa sababu hakunyimwa dhamana.
Mawakili hao waliitaka Mahakama hiyo itupilie mbali maombi hayo na
iwatake kufuata njia sahihi ya kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa.
Wakili Kadushi alitaja vifungu vya sheria na kutolea mfano wa hukumu zilizowahi kutolewa na zinazofanana na kesi hiyo.
Jopo la mawakili wa mshitakiwa chini ya wakili Peter Kibatala liliwasilisha maombi Mahakama Kuu kutaka Mahakama hiyo irejee upya uamuzi wa Mahakama ya chini kutokana na kwamba taratibu za uamuzi huo hazikuzingatiwa.
Wakili Kibatala aliomba Mahakama irejee upya uamuzi huo akidai kuwa Mahakama hiyo haikutenda haki, kwa sababu ikishatoa dhamana, haitakiwi kuishia hapo, lazima isimamie dhamana hiyo na kutoa
masharti yake.
Kwa pingamizi hilo, Lema alirudishwa mahabusu hadi Novemba 22 kesi hiyo itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
0 comments:
Post a Comment