Mery Kitosio, Arusha
Dk Harrison Mwakyembe |
WAZIRI wa Katiba
na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe, ameeleza kusikitishwa na baadhi ya nchi
za Afrika ambazo hazijasaini mkataba wa Itifaki wa kuanzishwa Mahakama ya
Haki za Binadamu akieleza kuwa kitendo hicho kinawanyima Watanzania fursa ya kupata
haki.
Alisema kati ya
nchi 54 za Afrika, ni 30 pekee ndizo zilizosaini Itifaki hiyo.
Alisema hayo juzi
wakati akizungumza kwenye sherehe ya miaka 10 ya kuanzishwa kwa Mahakama ya
Haki za Binadamu jijini hapa.
Alisema katika
kipindi hicho, wamepata mafanikio makubwa, lakini bado anasikitishwa na nchi
ambazo hazijakubali kusaini.
“Kati ya nchi 54
za Afrika ni 30 tu zilizokubali kusaini Itifaki, lakini naona hii inatokana na utashi wa kisiasa maana
mbona nchi ambazo zilikubali ikiwamo Tanzania hazijapasuka vipande ziko tu
vizuri?
“Bado sijaelewa
sababu za nchi hizo kukataa Itifaki hiyo. Naziomba ambazo hazijakubali zikubali ilikusudi hata
wananchi wao wawe na uhuru wa kupeleka kesi zao mahakamani,” alisema Dk
Mwakyembe.
Alisema pamoja
na Tanzania kuongoza kuwa na kesi nyingi za kulaumiwa, bado ipo kwenye moja ya
nchi zilizokubali kusaini Itifaki hiyo ingawa bado ipo katika kipengele cha kuwezesha
wananchi mmoja mmoja kupeleka kesi zao mahakamani hapo.
Jaji mstaafu wa Mahakama
ya Haki za Binadamu, Jaji Augustino Ramadhani alisema ni jukumu la Serikali
ya Tanzania kujenga Mahakama eneo la Laki Laki, Kisongo, kwani ni kubwa na linakidhi
mahitaji ya kujengwa Mahakama hiyo.
0 comments:
Post a Comment