Emeresiana Athanas
MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji
(Ewura), imeanza kupitia maoni ya wadau kuhusu maombi ya Shirika la Umeme
Tanzania (Tanesco), kupandisha gharama ya umeme kwa asilimia 18.19 kuanzia
mwakani.
Akuzungumza Dar es Salaam jana, Kaimu
Mkurugenzi wa Umeme Ewura, Godfrey Chibulunje alisema maoni hayo yalikamilika
Novemba 25.
Alisema baada ya kuyapitia na
kuyachambua, yatafikishwa kwenye Bodi ya Mamlaka hiyo na hatimaye kutoa uamuzi
sahihi.
"Novemba 25 ndiyo ilikuwa mwisho wa
kukusanya maoni na tayari yameanza kupitiwa kisha yatafikishwa kwenye Bodi ya
Ewura ili kutoa uamuzi," alisema.
Aliongeza kuwa uamuzi huo utatangazwa
ndani ya mwezi huu ili kuhakikisha Januari bei mpya zinaanza kutumika.
Kwa mujibu wa Tanesco, maombi ya
mabadiliko ya gharama yaliwasilishwa Ewura, kulingana na agizo la kubadilisha
bei za umeme la mwaka huu lililoanza kutekelezwa Aprili.
Kwa mujibu wa agizo hilo bei hizo zinatumika
hadi Desemba 31 na hivyo Januari zinatakiwa bei mpya za umeme
kwa mujibu wa sheria.
0 comments:
Post a Comment