Jemah Makamba
Mahamoud Mgimwa |
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mahamoud Mgimwa ametaka Watanzania wawe na utaratibu wa kutembelea hifadhi na
sehemu za vivutio badala ya kuachia wageni peke yao.
Akizungumza Dar es Salaam jana, alisema
Watanzania wengi hawana kawaida ya kutembelea vivutio vya ndani ya nchi, jambo
ambalo linafanya wageni peke yao ndio waone uzuri wa nchi.
Mgimwa alisema Tanzania ina vivutio
vingi na vizuri vyenye kuvutia, lakini Watanzania wanashindwa kutembelea hata
sehemu za karibu na kuachia wageni kufurahia.
Alisema wanatakiwa wawe na kawaida ya kuchanga
fedha na mwisho wa mwaka watembelee sehemu tofauti za utalii, kwani bei za
kuingia sehemu za utalii ni za kawaida, hivyo wana uwezo wa kumudu na kwenda
kuona vivutio na uzuri wa nchi.
Aidha alisema kuelekea kilele cha Wiki
ya Utalii kitakachofanyika Iringa watahamasisha Watanzania wengi, wajifunze
kuwa na kawaida ya kujua vivutio na hifadhi za wanyama badala ya kuachia wageni
wanaotoka nchi za mbali kuona uzuri wa nchi yao huku wao wakiwa hawajawahi
kabisa kutembelea hifadhi yoyote.
0 comments:
Post a Comment