Dotto Mwaibale
Balozi wa China nchini Tanzania, Dk Lu Youqing |
UJUMBE wa watu sita kutoka Chama cha Kikomunisti cha
China (CPC) uko nchini kwa ziara ya siku saba kujifunza shughuli zinazofanywa
na CCM.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa
CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida alisema ujumbe huo unaongozwa
na Mkurugenzi wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo
cha Viongozi wa Chama hicho, Jia Bo.
Madabida alisema lengo la ziara hiyo ni kudumisha
ushirikiano baina ya Tanzania na China ulioasisiwa na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Nyerere na Baba wa Taifa la China, marehemu Mao Tse-Tung.
Alisema ujumbe huo ambao utatembelea Temeke na Zanzibar
uliwasili nchini baada ya ziara ya baadhi ya makada wa CCM waliokwenda China na
kujifunza mambo mbalimbali ambayo ujumbe huo utapenda kujua kama wameyafanyia
kazi.
Mratibu wa Masuala ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM,
Dk Pindi Chana alisema ujio wa viongozi wa chama hicho ni matunda ya
ushirikiano wa Tanzania na nchi mbalimbali duniani.
"Ujio wa wenzetu hawa kutoka China ni matunda ya
ushirikiano kati yetu na nchi zingine kama Zimbabwe, Afrika Kusini, Angola,
Cuba na zinginje za Ulaya hasa katika
siasa za kijamaa," alisema Chana.
Alisema China wako karibu bilioni moja na wamepiga hatua
katika maeneo mbalimbali hivyo ujio wao nchini ni fursa kwao kujifunza mambo
yetu na sisi kujifunza kwao kutokana na hatua ya kiuchumi waliyopiga..
0 comments:
Post a Comment