John Banda, Dodoma
George Simbachawene |
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi
George Simbachawene amesema kuwa kila mhitimu wa Chuo cha Serikali za Mitaa anatakiwa
kupewa mafunzo maalumu ya ukakamavu ili kuweza kukabiliana na wahalifu wanapoanza
kufanya kazi na kujitegemea.
Waziri huyo aliyasema hayo wakati
alipokuwa akiwahutubia wahitimu 700 katika mahafali ya nane ya chuo hicho kilichopo
katika Kata ya Homboro, manispaa ya Dodoma mwishoni mwa juma.
Waziri huyo alisema iko haja kwa wanafunzi
wanaohitimu chuoni hapo kupata mafunzo ya ukakamavu kwa sababu wakishaajiriwa wataongoza
askari wa akiba au waliopo katika kupambana na wala rushwa, majambazi na wakati
mwingine watakiwa kutoa maelekezo ya namna yakuwakata watuhumiwa wa makosa ya
jinai.
“Kutokana
na mfumo wa kazi mnaokwenda kuifanya ni vema mkapata mafunzo yanayoendana na
maswala ya usalama pia ukakamavu, mjue hata ABC za silaha ili atakapokuwa
amesikia imepigwa ajue namna ya kukabiliana na walengwa,
Wiki za mwisho waje JKT kuwapa mafunzo
maalumu ili wakitoka wawe na ukakamavu na mbinu za kutosha za usalama ili
wanapokuwa kazini waweze kupambana na wahalifu hata kama wanatumia silaha na
wale waliovunja sheria kwa kufanya makosa ya jinai”, alisema
Aidha alisema wahitimu hao ambao wanaandaliwa
kwa ajili ya kuwa watendaji wa kata na vijiji ambao pia wanakuwa wenyeviti wa
kamati za shule hivyo si watu wa kawaida hivyo ni vema wakapata ujuzi huo ili
waweze kufanya ueledi wao.
0 comments:
Post a Comment