Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema atampiga
marufuku Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kufanya mikutano
ya kisiasa Tanzania Bara kama hatamtambua kuwa mwenyekiti halali wa chama
hicho.
Lipumba alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza na
viongozi wa CUF kwenye mkutano wa ndani mkoani Geita.
Ziara ya Lipumba imefanyika wakati Maalim Seif akiwa amesambaza
barua kwa viongozi wa CUF wa wilaya zote nchini akiwataka wasishirikiane na Profesa
Lipumba huku akionya atakayekaidi atachukuliwa hatua.
“Kama Maalim Seif hatambui kuwa mimi ni mwenyekiti wake, huku
mimi nikimtambua kuwa Katibu Mkuu wangu, basi naye tutamzuia kufanya mikutano
ya kisiasa Tanzania Bara,” alisema Lipumba.
Profesa Lipumba alisema hana tatizo na wananchi wa
Zanzibar wala kiongozi wa upinzani atakayetetea watu hao na kuongeza kuwa yeye
amekuwa mstari wa mbele kutetea Wazanzibari.
“Mimi natambua kuwa ndiye mwenyekiti halali wa chama hiki
na mwenye mamlaka ya kumwondoa mwenyekiti au katibu ni mkutano mkuu wa chama na
lazima theluthi moja ya wajumbe watoke Bara na theluthi nyingine Zanzibar,
lakini mkutano huo haukufanyika wala muhtasari haupo,” alisema Profesa Lipumba.
Alieleza kwamba kwa sasa yeye na wana CUF wengine
wamejipanga kukijenga chama hicho.
Mwenyekiti huyo pia alizungumzia suala la Muungano akisema
ni muhimu kwa usalama wa nchi na Taifa kwa ujumla.
Alisema ili kulinda Muungano kuna mahitaji muhimu ya kuwa
na vyama vyenye nguvu vitakavyokuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya wananchi
wa pande hizo mbili.
Lipumba alisema amefika wilayani hapa akitoka Urambo
kwenye msiba wa Spika wa Bunge la Tisa, marehemu Samuel Sitta ambapo pia aliongea
na baadhi ya viongozi wa chama hicho.
“Tumeifika Kahama kuzungumza na viongozi wa hapa na wa wilaya
jirani, dunia ina changamoto kubwa katika masuala ya demokrasia na kujenga
utawala bora kwa baadhi ya viongozi,” alisema Lipumba.
Hata hivyo, akizungumzia kauli hiyo ya Lipumba ….(Itaunganishwa
na kauli ya Maalim au msaidizi wake)
0 comments:
Post a Comment