Diwani Athuman |
RAIS John Magufuli amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athuman, kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
wa Kagera.
Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,
Gerson Msigwa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, ilieleza kuwa uteuzi wa Athuman
unaanza mara moja.
Mwishoni mwa mwezi uliopita, Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Athuman katika nafasi yake ya DCI, katika
taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, bila kueleza
sababu.
Kijazi katika
taarifa hiyo, alisema Athuman aliteuliwa kushika nafasi hiyo Mei mwaka jana,
akitokea nafasi ya Kaimu Kamishna wa Kamisheni ya Intelijensia ya Jinai, atapangiwa
kazi nyingine na uteuzi wa Mkurugenzi mpya wa Makosa ya Jinai utatangazwa
baadaye.
Mbali na uteuzi huo, Rais Magufuli pia alifanya uteuzi wa
wenyeviti wa bodi za taasisi tano za Serikali, ambapo aliyekuwa Waziri Mkuu,
Jaji Joseph Warioba, aliteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
(SUA).
Kwa mujibu wa taarifa ya Msigwa, uteuzi wa Jaji Warioba
aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika Serikali ya Awamu
ya Nne, ulianza Jumatano.
Uteuzi mwingine uliofanyika ni wa Mwenyekiti wa Bodi ya
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), nafasi aliykabidhiwa Dk Jones Kilimbe,
huku aliyekuwa Mbunge wa Dole na Mwenyekiti wa Bunge, Sylvester Mabumba,
akiteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA. Uteuzi huo ulianza juzi.
Bodi nyingine iliyopata uongozi ni ya Shirika la Uhandisi
na Usanifu Mitambo (Temdo), ambapo Profesa Patrick Makungu, aliteuliwa kuwa
Mwenyekiti katika uteuzi ulioanza Jumatano.
Rais Magufuli
pia alimteua Martin Madekwe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi
katika tangu juzi huku Profesa Raphael Chibunda, akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wa
Baraza la Wakurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Kitropiki
Tanzania (TPRI).
0 comments:
Post a Comment